Matumizi na uuzaji wa Tramadol( )
Question
Ni ipi hukumu ya kuuza na kutumia Tramadol[1] bila idhini ya daktari?
[1] Tramadol ni dawa iliyotengenezwa kwa kiasi fulani cha madawa ya kulevya, inatumika chini ya usimamizi wa madaktari ili kutuliza maumivu na kusaidia kutibu baadhi ya magonjwa.
Answer
Sharia ya Kiislamu inakataza matumizi ya kitu chochote kinacholewesha akili na kusababisha kupoteza fahamu, na dawa za kulevya zinachukuliwa sawa na pombe katika Sharia ya Kiislamu, kama alivyosema Mtume (S.A.W) "Kila kile kinacholewesha ni pombe, na kila pombe Haramu." Na akasema Mtume (S.A.W): "Kile kinacholewesha kwa wingi kimeharamishwa kwa uchache."
Uislamu pia unakataza matumizi ya chochote kinachoharibu afya ya binadamu na kuumiza mwili. Mwenyezi Mungu Anasema: {wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo.} [Al-Baqarah: 195], na Mtume (S.A.W): amesema "Usidhuru wala usijidhuru."
Imethibitishwa kitabibu kwamba Tramadol inaweza kusababisha madhara ikiwa itatumika bila usimamizi wa kitabibu. Kwa hivyo, ni haramu kwa mtu kutumia Tramadol ili kujisikia furaha isiyo ya kawaida au kulewesha akili na hisia zake, kama vile pombe.
Pia ni haramu kisharia kwa wafamasia kuuza Tramadol bila agizo la daktari bingwa na kwa kiasi maalumu, na ni lazima watii kanuni na Sharia zinazosimamia taaluma yao.
Maelezo
Sharia ya Kiislamu inakataza matumizi ya kitu chochote kinacholewesha akili na kusababisha kupoteza fahamu. Mwenyezi Mungu anasema: {Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa} [Al-Ma'idah: 90]. Hukumu ya madawa ya kulevya katika Sharia ya Kiislamu ni sawa na ile ya pombe, kwa kauli ya Mtume (S.A.W): (Kila kile kinacholewesha ni pombe, na kila pombe ni haramu). Imepokelewa na Muslim. Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesma: (Kila kitu kinacholewesha kwa kiasi kikubwa ni haramu kwa kiasi kidogo) .
Sharia ya Kiislamu pia inakataza matumizi ya chochote kinachoharibu afya ya binadamu na kumdhuru mwili. Mwenyezi Mungu Anasema: { wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo } [Al-Baqarah: 195], na akasema: {Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni } [An-Nisa: 29], Aya hizi mbili zinakataza kujidhuru na kujiingiza katika maangamizi, na zinatuamrisha kujikinga na hatari na madhara. Mtume amesema (S.A.W): (Usidhuru wala usijidhuru.").
Imethibiti kitabibu kwamba Tramadol ina madhara hatari yanayotokana na matumizi yake bila usimamizi wa kitabibu katika dozi fulani, madhara haya ni pamoja na:
Uzito katika utendaji wa mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na kupungua kwa choo.
Kizunguzungu, kichefuchefu, na kutapika.
Ugumu wa kukojoa, hasa kwa kutumia dozi kubwa kupita kiasi.
Mapigo ya moyo ya chini na shinikizo la damu la chini.
vidonda vya tumbo kwa kutumia dozi kubwa mno na matumizi ya kupita kiasi.
Kuona kizunguzungu na ugumu wa kuona, jambo ambalo huathiri vibaya shughuli za kila siku.
Kupumua kwa tabu, kwani husababisha kupooza kwa mfumo wa upumuaji.
Kutetemeka kwa matumizi ya dozi kubwa.
Kuitumia pamoja na dawa za vidonda vya tumbo huongeza muda wa dawa kukaa mwilini na kuongezaka madhara yake.
Kuitumia pamoja na baadhi ya dawa za kutibu msongo wa mawazo huongeza uwezekano wa kutetemeka.
Kuitumia pamoja na pombe huleta mfadhaiko kwenye mfumo wa neva.
Kumeza dozi kubwa kupita kiasi kunaweza kusababisha kusimama kwa moyo na kusababisha kifo.
Kuitumia kutibu kuwahi kufika kileleni kunaweza kuwa na manufaa, lakini matumizi ya mara kwa mara husababisha kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa na kudhoofika kwa uwezo wa uume kusimama. Tramadol pia husababisha ulemavu na uharibifu wa mbegu za kiume, na hivyo kusababisha uharibifu na madhara ya mbegu za kiume hivyo kumdhuru mtoto alie tumboni.
Baada ya maelezo haya, ni lazima tufafanue hukumu kadhaa za kisharia zinazohusu Tramadol, ambazo ni kama zifuatazo:
Kwanza: Ni marufuku na ni haramu kwa mtu kutumia Tramadol bila usimamizi wa kitabibu na katika dozi maalumu.
Pili: Ni haramu kisharia kutumia Tramadol ili kupata hisia za furaha isiyo ya kawaida au kulewesha akili na hisia, kwa kulinganisha na pombe.
Tatu: Ni haramu kwa mfamasia kuuza Tramadol bila idhini au agizo la daktari, na kwa dozi maalumu, na kunapasa kwake kufuata sheria za kazi yake.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
