Mwanamke Kufunika Miguu katika Swala
Question
Ni ipi hukumu ya mwanamke kufunika miguu yake katika Swala? Je! Swala yake inakubalika miguu yake ikiwa wazi?
Answer
Ni wajibu kwa mwanamke kufunika mwili wake wote wakati wa Swala isipokuwa nyuso na viganja viwili, imepokewa kutoka kwa Omar bin Al-Khattab (R.A) amesema: "Mwanawake anaswali na nguo tatu: Gauni, mtandio, na sketi."
Kuhusu mwanamke kufunika miguu yake wakati wa Swala, Wanazuoni wametofauti juu ya suala hili:
Baadhi yao wanasema kwamba ni wajibu kufunika miguu, kwa kutegemea Hadithi ya Umm Salama (R.A) ambaye amesema kwamba mwanamke mmoja alimuuliza kuhusu nguo ambazo wanawake wanapaswa kuvaa wakati wa Swala, naye akajibu: "Anapaswa kuswali akiwa amevaa ushungi na gauni refu linalofunika sehemu za nyuma za miguu yake," ikimaanisha kuwa linafunika na kuficha sehemu za nyuma za miguu yake.
Wengine wanasema kwamba inaruhusiwa kufunua miguu yake, kwa sababu Sharia imeondoa uso, viganja viwili na miguu kutoka katika mapambo ya wanawake, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu Anavyosema: { wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika } [An-Nur: 31].
Maoni sahihi zaidi, ambayo ndiyo hukumu imetolewa Fatwa, ni kwamba inaruhusiwa kwa mwanamke kufunua miguu yake katika Swala, ili kumrahisishia na kuondoa ugumu wowote kwake. Akiswali miguu yake ikiwa haijafunikwa, Swala yake ni sahihi.
Maelezo
Ni lazima kisharia kwa wanawake kufunika miili yao katika Swala isipokuwa nyuso na mikono yao. Imepokewa kutoka kwa Aisha (R.A) kwamba Mtume (S.A.W) amesema: "Mwenyezi Mungu haikubali Swala ya mwanamke aliye baleghe isipokuwa avae mtandio." Imepokewa na Abu Dawood. imepokewa kutoka kwa Omar bin Al-Khattab R.A. kwamba amesema: "Mwanamke anapaswa kuswali akiwa amevaa nguo tatu: Gauni, mtandio na sketi."
Hadithi hizi za Mtume zilizopokelewa zinaashiria kwamba mwanamke anapaswa kufunika mwili wake wote katika Swala isipokuwa uso na viganja vyake.
Wanazuoni wa Fiqhi wametofautiana kuhusu wajibu wa wanawake kufunika miguu yao katika Swala, na kuwa na maoni kadhaa kama ifuatavyo:
Maoni ya kwanza: Mwanamke lazima afunike miguu yake wakati wa Swala, kwa kutegemea Hadithi ya Umm Salamah (R.A) Mwanamke mmoja alimuuliza kuhusu nguo ambazo wanawake wanapaswa kuvaa katika Swala, naye akasema: "Ana Swali akiwa amevaa ushungi na nguo ndefu inayofunika sehemu ya nyuma ya miguu yake," yaani ile inayofunika na kuficha sehemu ya nyuma ya miguu.
Maoni ya pili: Inaruhusiwa kwa wanawake kufunua miguu yake wakati wa Swala, kwa sababu Mwenyezi Mungu, Aliwaamrisha wajipambe wanapoenda msikitini kuswali, kama Alivyosema: {Enyi wanaadamu! Chukueni pambo lenu kwenye kila pahala wakati wa ibada, na kuleni, na kunyweni na wala msifanye ubadhirifu. Kwa hakika Yeye hapendi wanao fanya israfu } [Al-A'raf: 31], na Akasema: { wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika } [An-Nur: 31].
Imevuliwa katika mapambo ya mwanamke: uso, mikono, na miguu.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Hukumu iliyotolewa Fatwa ni kwamba kunajuzu kwa wanawake kufunua miguu yao wakati wa Swala, kwa mujibu wa maoni ya Wanazuoni waliosema hivyo, ili kurahisisha kwa wanawake na kuondoa uzito kwao. akiswali akiwa amefunua miguu yake, Swala yake ni sahihi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
