Hukumu ya Uchoraji
Question
Ni nini hukumu ya uchoraji katika Uislamu?
Answer
Uchoraji ni miongoni mwa sanaa nzuri ambazo zina athari njema katika kutuliza nafsi na kuifurahisha. Isitoshe, uchoraji unaweza kuelezea jambo fulani na kuonyesha athari yake katika jamii kwa namna ambayo maneno na hotuba zinaweza kushindwa kufanya hivyo.
Hukumu ya uchoraji kisharia umegawanyika katika aina tatu:
Uchoraji wa vitu visivyo na roho: Kama vile mandhari ya asili ya milima, miti, na mfano wa hivyo. Aina hii inajuzu kwa makubaliano ya Wanazuoni wote wala hakuna ubaya.
Uchoraji wa viumbe wenye roho (binadamu na wanyama) kwa namna ya kivuli au umbo lisilo na maelezo (silhouette): Ambapo sura na miondoko ya mchorwa haionekani wazi. Aina hii ya uchoraji inajuzu wala haina kizuizi.
Uchoraji wa viumbe wenye roho kwa sura na maelezo yaliyo wazi: Sawa mchorwa awe ni binadamu, mnyama, au ndege. Aina hii inajuzu kwa masharti yafuatayo:
a) Maudhui ya uchoraji yawe ni ya halali.
b) Mchorwa asiwe miongoni mwa vitu vinavyolingania kwenye machafu au kuchochea matamanio ya kingono.
Na hakuna kizuizi kisheria kwa baadhi ya watu kufanya kazi ya uchoraji wa binadamu, kuuza picha hizo, na kujipatia kipato kupitia kipaji hicho.
Maelezo
Uchoraji ni miongoni mwa sanaa nzuri ambazo zina athari nzuri katika kutuliza nafsi na kuifurahisha. Isitoshe, uchoraji unaweza kuelezea jambo fulani na kuonyesha athari yake katika jamii kwa namna ambayo maneno na hotuba zinaweza kushindwa kufanya hivyo.
Hukumu ya uchoraji kulingana na uhalali wake kisharia umegawanyika katika aina tatu:
Uchoraji wa vitu visivyo na roho: Kama vile mandhari ya asili ya milima, bahari, miti, nyota, na mfano wa hivyo. Aina hii ya uchoraji inajuzu kwa mwafaka wa wanazuoni wote wala haina kizuizi.
Uchoraji wa viumbe wenye roho kama binadamu na wanyama, lakini kwa namna ya kivuli (silhouette): Ambapo mchoraji haonyeshi maelezo ya sura ya mtu au mnyama, bali anachora kwa namna ambayo mtazamaji anatambua kuwa huyu ni binadamu, ndege, au mnyama. Aina hii ya uchoraji pia inajuzu wala haina kizuizi.
Uchoraji wa viumbe wenye roho kwa namna inayonyesha maelezo ya mchorwa kwa usahihi na ubora wa hali ya juu: Aina hii ya uchoraji inajuzu kisheria kama wanavyoona baadhi ya wanazuoni[1], lakini kwa masharti yafuatayo:
a. Uchoraji usiwe wenye kuchochea matamanio na hisia za kingono.
b. Maudhui ya uchoraji yasiwe ni mwili ulio uchi au tupu miongoni mwa tupu ambazo zimeamriwa kusitiriwa.
Tunapata faidia Kutokana na yaliyotangulia:
1- Rai sahihi (Rai inayokubaliwa zaidi) iliyochaguliwa na Ofisi Kuu ya kutoa Fatwa ya Misri: Inajuzu kuchora viumbe vyenye roho kwa sura na maelezo yaliyo wazi, sawa mchorwa awe ni binadamu, mnyama, au ndege. Hii ni kwa sharti kwamba maudhui ya uchoraji yawe yanajuzu kisharia, na mchorwa asiwe miongoni mwa vitu vinavyolingania kwenye machafu au kuchochea matamanio ya kingono.
2- Haikubaliki kwa yeyote kumpinga au kumkosoa yule anayechora viumbe vyenye roho kwa kuzingatia masharti yaliyotajwa; kwani kanuni ya kisharia inathibitisha kuwa: "Hakuna kukemea katika hukumu ambayo Wanazuoni wametofautiana.
3- Hakuna kizuizi kisharia kwa baadhi ya watu kufanya kazi ya uchoraji wa binadamu, wanyama wafugwao, na viumbe vingine, kisha kuuza picha hizo na kujipatia kipato kupitia kipaji hicho.
[1] Huu ni msimamo wa madhehebu ya Malikia, Manh Al-Jalil, Sharh Mukhtasar Khalil (3/ 529).
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
