Kuwapongeza wakristo katika Siku ku...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuwapongeza wakristo katika Siku kuu zao

Question

Ni nini hukumu ya  kuwapongeza wakristo katika siku kuu zao?

Answer

Uislamu ni dini inayoagiza wema na kuzungumza kwa upole na watu wote. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Waambie waja wangu waseme maneno mazuri} [Al Israa 53]. Na pia Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {nasemeni na watu kwa wema} [Al Baqarah 83]. Aya hii Tukufu inawahimiza Waislamu kuwa wema kwa matamko na matendo pamoja na watu wote, bila kujali imani au akida zao.

Sharia ya Kiislamu imeamrisha kueneza amani miongoni mwa watu wote, kwani dini ya Uislamu ni dini ya amani na rehema kwa viumbe vyote vya Mwenyezi  Mungu. Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu} [Al Mumtahinah 8]. Kwa hiyo, inaruhusiwa kwa Muislamu kuwapongeza wasio Waislamu katika sikukuu zao na minasaba yao, na hakuna ubaya wowote. Bali, inachukuliwa kuwa kitendo cha wema na kudumisha uhusiano, ambacho Sheria tukufu imetuamuru kukifanya katika kutendeana na wasio Waislamu.

Maelezo

Uislamu ni dini inayoagiza wema na kuzungumza kwa upole na watu wote. Mwenyezi Mungu Mtukufu amefafanua kwamba upole ni miongoni mwa sifa za waja wake, akasema: {Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanaotembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama!} [Al Forqaan 63], Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Waambie waja wangu waseme maneno mazuri} [Al Israa 53].

Basi, Maneno mazuri yana athari kwenye mioyo na akili, kwa hiyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwahimiza, katika agano ambalo Mwenyezi Mungu Mtukufu alilichukua kutoka kwa Wana wa Israeli, aliwaambia: {nasemeni na watu kwa wema} [Al Baqarah 83]. Aya hii Tukufu inawahimiza waislamu kuwa wema kwa matamko na matendo pamoja na watu wote, bila kujali imani au akida zao.

Aagizo la kuzungumza kwa upole haliishii pamoja na Waislamu pekee, bali linaenea kwa wengine. Muislamu anatakiwa kuwa mpole na mkarimu kwao, ili Muislamu awe mfano wa kuigwa kila wakati na mahali.

Kuwapongeza wasio Waislamu katika sikukuu zao na minasaba yao inaruhusiwa katika sheria ya Kislamu kwa sababu kadhaa kama zifuatazo:

Pongezi hizo zinazingia chini ya kundi la jumla la wema unaoamriwa; katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu} [Al Mumtahinah 8]. Aya tukufu inawaongoza Waislamu, na hata wasio Waislamu, mradi tu hawaonyeshi uadui dhidi ya Waislamu na Uislamu; kutoka kwa Asma’ Bint Abi Bakr R.A., amesema: “Mama yangu alikuja kwangu akitaka kunitembelea wakati wa Mtume S.A.W., nikamwuliza Mtume S.A.W. : Je, nidumishe uhusiano naye? Akasema: Ndiyo.”  Ibn Uyaynah amesema:  Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha kuhusu hilo: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita} [Al Mumtahina 8], imepokelewa na Al Bukhariy.

Pongezi hizo ni aina tu ya salamu ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu hajaitofautisha katika kutoa, na kuitikia kati ya Waislamu na wasio Waislamu; Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na mnapo amkiwa kwa maamkio yoyote, basi nanyi itikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo, au rejesheni hayo hayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuhisabu kila kitu} [An Nisaa 86]. Ibn Abbas R.A. akasema: "Ikiwa mtu yeyote kutoka katika viumbe vya Mungu atakusalimini, mrudishieni salamu, hata kama ni Myahudi, Mkristo, au muabudia moto."[1]

Huo ndio utekelezaji sahihi wa kivitendo wa Uislamu, ambao unawawajibisha wafuasi wake kuishi pamoja na watu wa dini zingine, na kuwa na haki na wajibu sawa na Waislamu. Na kwamba wanapaswa kuwa na haki na wajibu sawa na Waislamu.

Tunapata faida kutokana na yalitangulia:

Sharia tukufu inawaamuru Waislamu kuwatendea watu wote kwa wema bila kutofautisha kati ya Waislamu na wasio Waislamu.

Sharia ya Kiislamu imeamuru kutoa salamu mwa watu wote, kwani dini ya Uislamu ni dini ya amani na huruma kwa viumbe vyote vya Mungu.

Inaruhusiwa kwa Muislamu kuwapongeza wasio Waislamu katika sikukuu zao na minasaba yao, na hakuna ubaya wowote. Bali, inachukuliwa kuwa kitendo cha wema na kudumisha uhusiano, ambacho Sharia tukufu imetuamuru kufanya katika kutendeana na wasio Waislamu.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi

 

[1] - Imepokelewa na Ibn Abi Shaibah katika kitabu cha Al Musanaf, (250/5)

Share this:

Related Fatwas