Kufanya kazi katika Hoteli au Migahawa inayouza pombe
Question
Ni ipi hukumu ya kufanya kazi katika Hoteli au Migahawa inayouza pombe?
Answer
Haijuzu kwa Muislamu kufanya kazi au kujipatia kipato kutokana na biashara ya pombe, au kuwahudumia kwa pombe wateja na mfano wa hayo katika aina zote za miamala inayosaidia kutumiwa, na mtendaji wa hilo amelaaniwa; imepokelewa kutoka kwa Abdullah Ibn Umar (R.A), kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema: ((Mwenyezi Mungu amelaani pombe, na mnywaji wake, na mnyweshaji wake, na muuzaji wake, na mnunuzi wake, na mkamuaji wake, na mkamuliwa wake, na mbebaji wake, na kinachobebewa)).
Ama ikiwa kipato cha Muislamu na chumo lake linatokana na sehemu hiyo ambayo pombe huuzwa kwa wateja kama baadhi ya Hoteli au Migahawa, basi ni wajibu kwake ajiepushe na kuwaandalia wateja.
Na tunamuusia anayefanya kazi katika sehemu hizo aombe kwa wahusika kazini kuhamishiwa nyanja nyingine, kama huduma za vyumbani, au kuweka oda (za makazi hotelini), au mapokezi, au ulinzi, au kwingineko katika vitengo vilivyohalalishwa ambavyo havihudumii mambo yaliyoharamishwa.
Maelezo
Imethibitishwa kisharia uharamu wa kutumia kila kinacholevya akili ya mwanadamu na kuondosha fahamu yake, iwe kiasi anachotumia mtu ni kidogo au kingi; Mwenyezi Mungu anasema: {Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa. Hakika Shet'ani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha? [Al-Ma'idah: 90-91]. Na imepokelewa kutoka kwa Abdullah Ibn Umar (R.A) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema: ((Kila chenye kulevya ni pombe, na kila pombe ni haramu)) Imepokelewa na Muslimu.
Na imepokelewa kutoka kwa Abdullah Ibn Umar (R.A) pia, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema: ((Mwenyezi Mungu ameهlaani pombe, na mnywaji wake, na mnyweshaji wake, na muuzaji wake, na mnunuzi wake, na mkamuaji wake, na mkamuliwa wake, na mbebaji wake, na kilichobebewa[1])).
Hivyo dalili hizi na maandiko haya ya kisharia yanaonesha uharamu wa kutumia pombe na vileo vyote vinavyoondosha akili na kupoteza fahamu, na haramu kuiuza, kuinunua, kuibeba, kuitengeneza, na aina zote za miamala inayosaidia kuinywa.
Uislamu pia umehimiza kufanya kazi na jitihada za kutafuta riziki na kuifanya hiyo kuwa ni faradhi, imepokelewa kutoka kwa Anas Ibn Malik (R.A), kutoka kwa Mtume (S.A.W) amesema: ((Kutafuta cha halali ni wajibu kwa kila Muislamu))[2]. Na Mtume (S.A.W) ametuusia tufanye kazi na tujichumie kutokana na katika halali; kutoka kwa Al-Miqdam (R.A), kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema:
«Hajala yeyote chakula kamwe kilicho bora kuliko kula kutokana na kazi ya mkono wake, na hakika Nabii wa Mwenyezi Mungu Daudi (A.S) alikuwa akila kutokana na kazi ya mkono wake[3]»[4].
Lakini kuna baadhi ya watu wanafanya kazi katika Hoteli au Migahawa inayotoa huduma ya pombe kwa wateja, na hukumu yao ni hivi:
Kwanza: Haijuzu kwa Muislamu kufanya kazi au kujipatia kipato kutokana na biashara ya pombe, au kuwahudumia wateja na mfano wa hayo katika aina zote za miamala inayosaidia kuinywa, na mtendaji wa hilo amelaaniwa[5] kama ilivyooneshwa na Hadithi ya Mtume.
Pili: Ikiwa kipato cha Muislamu na chumo lake linatokana na sehemu hiyo ambayo pombe hutolewa kwa wateja kama baadhi ya Hoteli au Migahawa, basi ni wajibu kwake ajiepushe na kuwahudumia wateja.
Tatu: Tunamuusia anayefanya kazi katika sehemu hizo aombe kwa wahusika kazini kuhamishiwa nyanja nyingine, kama huduma za vyumbani, au kuweka oda (za makazi), au mapokezi, au ulinzi, au kwingineko katika vitengo vilivyohalalishwa ambavyo havitoi mambo ya haramu.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Kwamba kufanya kazi katika nyanja ya pombe kwa kuuza, kutengeneza, kuibeba, kuhudumia wateja na mengineyo katika aina zote za miamala inayosaidia kuinywa ni jambo haramu kisharia, na mtendaji wa hilo anastahiki adhabu na kufukuzwa katika rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kufanya kazi katika sehemu hizo zinazotoa pombe kwa wateja kama baadhi ya Hoteli na Migahawa kunajuzu kisharia kwa sharti la kujiepusha kuhudumia pombe hizo na nyinginezo katika mambo ya haramu kwa wateja au kujishughulisha nazo kwa namna yoyote.
[1] Imepokelewa na Abou Dawoud
[2] [2] ((Anakula kutokana na kazi ya mikono yake)): Kutokana na mapato yake na matokeo ya kazi ya mikono yake.
[3] ((Anakula kutokana na kazi ya mikono yake)): Kutokana na mapato yake na matokeo ya kazi ya mikono yake.
[4] Imepokelewa na Al-Bukhari.
[5] "Amelaaniwa ": Maana yake ni mwenye kustahiki adhabu na kufukuzwa katika rehema ya Allah.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
