Kuchelewa kugawa Urithi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuchelewa kugawa Urithi

Question

Ni ipi hukumu ya kisharia kuhusu kuchelewesha kugawa urithi kwa sababu ya mmoja wa warithi kuchelewesha na kutowawezesha warithi wengine kupata fungu lao la urithi?

Answer

Kisharia, urithi baada ya kifo cha mrithiwwa ni haki ya warithi wote kwa pamoja -wanaume kwa wanawake, wadogo kwa wakubwa- Kila mrithi anastahili fungu lake baada ya kukatwa gharama za mazishi, kulipa madeni, kutekeleza wasia, kafara, nadhiri na mambo kama hayo.

Haijuzi kwa mrithi yeyote kuzuia warithi wengine kupata mafungu yao yaliyokadiriwa kisharia kwa kuwanyima au kuchelewesha. Hairuhusiwi kwa mmoja wao kujichukulia mamlaka ya kutumia urithi bila idhini ya warithi wengine; hivyo, kuzuia mgawanyo au kuuchelewesha bila udhuru au idhini ni haramu kisharia. Ushahidi wa hilo ni kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na kimbilieni maghfira ya Mola wenu, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi...} [Al-Imran: 133]. Aya hii inaamrisha kuharakisha mambo yanayoleta maghfira, na miongoni mwa sababu kuu za kuingia Peponi ni kutekeleza haki za watu sawa sawa ziwe haki za Mwenyezi Mungu au za watu.

Maelezo

Urithi ni haki aliyoiweka Mwenyezi Mungu kwa ajili ya warithi. Imethibiti kisharia kwamba umiliki wa mali na alichokiacha marehemu inahamia kwa warithi mara tu baada ya kifo cha mwenye mali kwa sababu uhusiano wa marehemu na mali hizo na vitu vingine alivyokuwa akivimiliki katika uhai wake unakatika; Imepokewa kutoka kwa Anas bin  Malik (R.A) amesema: Mtume (S.A.W). amesema: (Vitu vitatu humfuata maiti (kaburini), viwili hurejea na kimoja hubaki naye: hufuatwa na familia yake, mali yake na amali zake. familia na mali hurejea, na hubaki amali zake)[1].

Mali iliyoachwa na marehemu ni haki ya kila mrithi mwanamke na mwanamume, mtoto na mkubwa, kila mrithi ana haki ya  fungu lake baada ya mambo yafuatayo:

Kukatwa gharama za maaandalizi ya mazishi ya marehemu.

Kulipa madeni ya marehemu ikiwa alikuwa anadaiwa.

Kutekeleza kafara na nadhiri ikiwa alikuwa nazo.

Kutekeleza wasia wake ndani ya mipaka ya thuluthi moja (1/3), au zaidi ya hapo kwa ridhaa ya warithi wote.

Ama Hukumu kwa anayechelewesha mgawanyo kwa masilahi binafsi pasi na ridhaa za warithi wengine, ni kama ifuatavyo:

Kwanza: Ni haramu kuchelewesha kugawa urithi kwa wenyewe bila haki ya kisharia. Sharia tukufu imekataza hilo na kuliharamisha,  imepokewa Hadithi kutoka kwa Anas bin Malik (R.A) amesema: Mtume (S.A.W). amesema: ((Mwenye kuukimbia urithi wa mrithi wake, Mwenyezi Mungu atamkata urithi wake wa Peponi Siku ya Kiyama))[2]. Hadithi hii inaashiria uharamu wa kumnyima mrithi urithi wake[3].

Pili: Miongoni mwa sababu kuu za kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kuingia Peponi kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu au haki za watu au hata haki ya Nafsi, na kunaingia kutekeleza haki za warithi  na kuwapa kwa haraka  katika hilo kuna kuepuka kuzichelewesha bila udhuru au idhini Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na kimbilieni maghfira ya Mola wenu, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi...} [Al-Imran: 133].

Tatu: Immekuja katika sharia tukufu ushahidi wa uharamu wa kuchelewesha Mirathi kwa warithi pasi na haki, imepokewewa Hadithi kutoka kwa Abouhurayara  (R.A) amesema: Mtume (S.A.W.) amesema: ((Mwenye kukata urithi aliofaradhisha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Mwenyezi Mungu atamkatia urithi wa Peponi))[4]. Maana ya Hadithi ni kwamba kumnyima urithi mmoja ya warithi ni haramu; kwa sababu kutolewa ahadi ya adhabu katika kitu ni dalili ya uharamu wake, na kukata kulipokuja katika Hadithi kunaingia kuzuia urithi moja kwa moja, au kuchelewesha muda wake wa kupata haki yake pasi na udhuru  au idhini.

Nne: Warithi wana haki ya kutumia kile wanachostahili bila kuzuiliwa na yeyote. Imepokewa kutoka kwa Hibban bin Abou Jabla R.A. amesema Mtume (S.A.W). amesema: (Kila mmoja ana haki zaidi na mali yake kuliko mzazi wake, mtoto wake na watu wote)[5].

Hadithi hii ni ushahidi kwamba mwanadamu ana haki ya kutumia mali yake, na umikili wa mrithi unakuja baada tu ya kifo cha mrithiwa, kuzuia au kuchelewesha mgawanyo wa mali kwa mmoja wa warithi na kutumia mali  bila idhini ya warithi wengine  ni jambo ambalo halijuzu kisharia.

Tano: Kuzuia urithi au  kuchelewa kugawa urithi ni uvunjaji wa haki za wengine na ni kula mali za watu kwa batili. Mwenyezi Mungu Amesema: {Enyi mlioamini! Msiliane mali zenu kwa batili...} [An-Nisaa: 29]. Imepokewa kutoka kwa Abou Hurayra (R.A). amesema Mtume (S.A.W). amesema: "Mfilisika" (Muflis) katika umma wangu Siku ya Kiyama ni yule  ambaye atakuja na Sala na Saumu na zaka, na atakuja akiwa amemtukana huyu, na kumsingizia yule, na amekula mali ya huyu, na kumwaga damu ya huyu, na amempiga huyu, atapewa huyu katika mema yake, na huyu katika mema yake, mema yakeyakimuishia  kabla ya kulipwa madeni yake, yatachukuliwa mabaya yao na kutupiwa yeye, kisha atatupwa  Motoni.[6]))

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia::

Kuchelewesha mgawanyo kwa mmoja wa warithi bila udhuru au idhini ya warithi wengine ni haramu kisharia.

Yeyote aliyewahi kuchelewesha urithi bila ridhaa ya wenyewe lazima atubu kwa Mwenyezi Mungu na kuharakisha kurudisha haki hizo kwa wenyewe, hii ili waweze kupata fungu lao la mali ya urithi.

Kunajuzu kwa warithi kutumia kile wanachostahili kutoka kwenye urithi na hakuna dhambi kwao kufanya hivyo.

 

[1] Imepokelewa na Al Bukhary

[2] Imepokelewa na Ibnu Majah

[3] Faydh Al Kabeer, cha Minyawy.

[4] Imepokelewa na Al Bayhaqy

[5] Imepokelewa na Al Bayhaqy

[6] Imepokelewa na Muslim.

Share this:

Related Fatwas