Uimamu wa mtoto kwa mtoto mwenzake
Question
Ni ipi hukumu ya Uimamu wa mtoto kwa mtoto mwenzake katika Swala? Na je, inatofautiana ikiwa Swala ni ya faradhi au ya Sunna?
Answer
Uimamu wa mtoto kwa mwenzake katika Swala ni sahihi kisharia, iwe katika faradhi au katika Sunna, hususan iwapo itakuwa na maana ya kuwatia moyo watoto wa kiume kujizoesha nayo, na kuwatamanisha kuifikia daraja yake, kupata thawabu ya jamaa na kuizoea. Pamoja na kulizingatia hilo, ni lazima liandamane na kuwafundisha Swala na hukumu zake, kushikamana na nguzo zake na masharti ya usahihi wake.
Maelezo
Sharia tukufu imewahimiza baba na mama katika malezi bora ya watoto, na kuwalea katika malezi yanayojengeka juu ya maadili mema, na kutekeleza ibada na kufanya mema, na kuwafundisha mambo ya dini yao na kuwazoesha kwayo, na kupanda mbegu za dini katika nafsi zao ili ziwe sehemu ya maisha yao; imepokelewa kutoka kwa Jabir Ibn Samurah (R.A), kutoka kwa Mtume (S.A.W) amesema:
“Baba akimfundisha mwanawe – au mmoja wenu akimfundisha mwanawe – ni bora kwake kuliko kutoa sadaka kila siku nusu pishi.” (Imepokelewa kutoka kwa Imam Ahmad katika Musnad).
Na miongoni mwa mambo muhimu ambayo Sharia tukufu imewaamrisha wazazi kuwafundisha watoto wao ni Swala; Mtume (S.A.W) amesema:
“Mtoto akishajua mkono wake wa kulia na wa kushoto basi muamrishe kuswali.” (Imepokelewa kutoka kwa Al-Tabarani katika Al-Mu‘jam Al-Awsat na Al-Saghir).
Imepokelewa kutoka kwa Mama wa Waumini Aisha (R.A) amesema: “Tulikuwa tukichukua watoto katika kuttab (Vyuo vya Quran) ili watuswalishe katika mwezi wa Ramadhan, nasi tukiwatengenezea qaliyya (Mchuzi ulipikwa kwa nyama na maini ya ngamia) na khushkananj (Mkate uliotengenezwa na unga wa ngano na kukandwa na mafuta ya ufuta)” (Imepokelewa kutoka kwa Al-Bayhaqi katika Al-Sunan Al-Kubra na Fadha’il Al-Awqat).
Na Wanazuoni wengi wa Madhehebu ya Imamu Hanafi, Maliki, Shafi na Hanabilah wameona uimamu wa mtoto kwa mwenzake katika Swala za faradhi na Sunna ni sahihi.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
