Hija ya Mtoto Mdogo inaondoa ulazim...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hija ya Mtoto Mdogo inaondoa ulazima wa Hija

Question

Nilihiji na baba yangu nilipokuwa na miaka nane, je Hija yangu hiyo ni sahihi? Na je Hija hiyo inaondoa ulazima kuhiji baada ya kubaleghe au la

Answer

Hija katika utoto mtu hupata thawabu nyingi, lakini inakuwa ni Sunna, haitoshelezi Hija ya faradhi, na kunapasa kutekeleza Hija ya Faradhi baada ya kubaleghe kwa mwenyekuwa na uwezo.

Jibu kwa urefu

Wanazuoni wameweka masharti kadhaa  katika kutekeleza Hija na Umra, miongoni mwazo ni: Kubaleghe, pia wamekubaliana kwamba mtoto mdogo hana wajibu wa Kuhiji, kwa kutokalifishwa kwake kwanza, yeye si wajibu kwake mpaka abaleghe([1]).

Mtoto mdogo ingawa hana wajibu wa kuhiji, isipokuwa akihiji au atakapohijiwa kwa niaba yake, Hija yake inajuzu, awe mpambanuzi au si mpambanuzi, na hii ndio kauli ya Fatwa; kwa Hadithi ya Al-Saaib bin Yazid R.A. amesema: “Nilihiji na Mtume S.A.W. nikiwa na miaka saba” imetolewa na Imamu Bukhari katika Sahihi yake.

Na imepokewa kutoka kwa Abdillah bin Abbas R.A. kwamba Mtume (S.A.W) alikutana na watu eneo la Al-Rawhaa, akawauliza ni kina nani nyinyi? Wakasema Waislamu, wakasema, na wewe ni nani? Akasema: Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mwanamke mmoja akamnyanyua mtoto, akasema:  je, huyu anaweza kuhiji? Akasema: ndio na ana malipo” imetolewa na Imamu Muslim katika sahihi yake.

Imamu Al-Qadhy Al-Ihaaydh amesema: “hakuna tofauti katika ya Wanachuoni wakubwa katika kujuzu Hija ya mtoto mdogo”([2]).

Hija ya mtoto mdogo hata kama inajuzu na inakuwa sahihi isipokuwa haindoi wajibu atakapobaleghe; kwa Hadithi ya Abdullah Ibn Abbas R.A, kwamba Mtume amesema: “Mtoto yeyote aliyehiji, kisha akabaleghe, basi ni wajibu kwake kuhiji tena” imetolewaa na Al Tabarany katika Al Muujam Al aw’sat. na Al Qatii katika Alif Deenaar, na Al Bayhaqy naktika Al Suna kubraa na Al Sunan Al Sughraa.

Na imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas R.A. amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (S.A.W): “Kija mdogo atakapohiji kabla ya kubaleghe, kisha akabaleghe, basi ni wajibu kwake kuhiji tena” imetolewa na Saeed biin Ourouba katika Al-Manasik na tamko ni lake, na Ibn Khuzayma katika Sahihi yake, na Al-Hakim katika  Almustadrak.

Na wamekubaliana Wanazuoni kwamba Hija ya mtoto mdogo haimtoshelezi na Hija ya faradhi baada ya kubaleghe, pia atakapo baleghe ni wajibu wake kuhiji akiwa na uwezo; kwani hilo halitoshi kwa Hija ya Uislamu.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Wanazuoni wamekubaliana kuwa mtoto mdogo hatakiwi kuhiji; kwa kutokalifishwa kwake, Hija si wajibu kwake mpala abaleghe.

Hija ya Mtoto mdogo hata kama inajuzu na inakuwa sahihi, isipokuwa haiondoi ulazima wa Hija atakapobaleghe.

 

([1]) Al-Iqnaa cha Imamu Ibn Al Qattan, 1/247, Al-Mughny cha Imamu Ibn Qudaama, 3/213.

([2]) Ikmaal Al-Muallim, 4/441.

Share this:

Related Fatwas