Kuuza damu ya Udh’hiya kwenye viwa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuuza damu ya Udh’hiya kwenye viwanda vya mbolea

Question

Kuna taasisi ya misada inachinja Udh’hiya kila mwaka kwa idadi kubwa ya wanyama, baadhi ya viwanda vya mbolea vimetuma maombi ya kununua damu za wanyama hao, je, kuna juzu kwa wasimamizi wa taasisi hiyo kuuza damu ya Udh’hiya kwa viwanda?

Answer

Damu za Udh’hiya ni najisi na ni haramu kuuza, isipokuwa kunajuzu kuwapa wenye viwanda vya mbolea kwa kuchukua pesa kwa njia ya “kuondoa kunufaika (Raaf Alyad An Ikhtisaas) na hilo ikithibiti manufaa yake katika kutengeneza mbolea ambayo itapelekea maendeleo ya kilimo, kutokuwa na madhara kutokana na hiyo mbolea kwa njia yoyote, iwe kwa mwanadamu, mmea au mazingira, hapo kutakuwa hakuna ubaya kisharia.

Maelezo

Udh’hiya ni ibada katika ibada za Kiislamu, Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: (Na ngamia wa sadaka tumekufanyieni kuwa ni kudhihirisha matukuzo kwa Mwenyezi Mungu)[Al-Haj: 36] na ibada hii ni katika ibada kubwa kwa mja kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya kuchinja na masiku ya Tashriiq. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: (Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya nyama hoa alio waruzuku. Basi kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri)[Al-Haj: 28].

Imepokewa Hadithi kutoka kwa mama wa Waumini Aisha R.A. kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Hakutenda mwanadamu amali inayopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu siku ya kuchinja kuliko kumwaga damu ya mnyama, mnyama huyu atakuja siku ya Kiama na pembe zake, na nywele zake na kwato zake, na hakika damu inafika kwa Mwenyezi Mungu katika sehemu, kabla ya kumwagika ardhini, basi zisafisheni nafsi kwa kuchinja” imetolewa na Imamu At-Tirmidhy katika Sunanih.  

Damu ya Udh’hiya ni najisi kwa makubaliano ya Wanazuoni wa Fiqhi, nayo ni nadamu iliyomwagika iliyoharamishwa katika kauli ya Mwenyezi Mungu: (Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho harimishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayo mwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu ... )[Al-Anaam: 145]

Wanazuoni wa Fiqhi wamekubaliana pia juu ya uharamu wa kuuza damu([1]); kwa Hadithi ya Ibn Abbas R.A. kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Mwenyezi Mungu Amewalaani Mayahudi, wameharamishwa mafuta ya mnyama wakayauza, na wakala thamani yake, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwaharamishia watu kitu, anawaharamishia na thamani yake”. Imetolewa na Imamu Ahmad katika Musnadih.

Na imepokewa Hadithi kutoka kwa Abu Juhayfa R.A. amesema: nimemuona baba yangu akisema: “Hakika Mtume (S.A.W) amekataza thamani ya damu, na thamani ya mbwa, na kula riba na kuilisha, na kuchora na kuchorwa tatuu.” Imetolewa ba Imamu Bukhari katika sahihi yake, na katika Hadithi hii kunachukuliwa uharamu wa kuuza damu.

Pia ni Haramu kuuza damu ya Udh’hiya na wala hakufai kuingia mkataba wa kuiuza, bali kunapasa kumwaga namu hii najisi na kujiepusha nayo kwa kuwa ni najisi.

Wataalamu wakiona faida ya damu hii iliyomwagika kuwa ina manufaa ya kutengeneza mbolea kwa faida ya kilimo au kuboresha aina ya kilimo, pamoja na kuthibiti kutokuwepo madhara kwa mwanadamu au kilimo au mazingira katika matumizi ya mbolea hiyo, na hilo likawa chini ya usimamizi wa vyombo husika, na ikawa katika masharti ya kuiuza ni kuwa twahara, damu ya Udh’hiya ni najisi kwa makubaliano ya Wanazuoni, basi hila ya kisharia katika kufaidika na damu hizi ni: Kutofanyika hilo kwa njia ya kuuza na kununua, bali kwa njia ya taasisi husika kuchukua pesa kwa kuruhusu viwanda vya mbolea kuchukua damu katika uhusika wa jumuia kuingia kwake katika kuhusika yenyewe, na hili linajulika kwa Wanazuoni wa Fiqhi “kuondoa kunufaika (Raaf Alyad An Ikhtisaas)”. Muamala huu unatofautiana na kuuza, na unatofautiana nao katika kuthibiti dhamana kwa mnunuzi kwa mkataba tu hata kama hakujatokea kukabidhiana, kwa kuwa dhamana katika kuuza unakuwa kwa muuzaji mpaka atakapomkabidhi bidhaa mnunuzi.

Hivyo basi kitendo cha taasisi katika ya Udh’hiya kinakuwa ni kujiondoa na “kuondoa kunufaika (Raaf Alyad An Ikhtisaas” kwa pesa na si kwa njia ya kuuza au kumiliki.

Na tofauti iliyopo kati ya kumiliki na kunufaika: ni kwamba milki inafungamana na vitu na manufaa, na kunufaika kuna kuwa katika manufaa tu, na mlango wa kunufaika ni mpana”([2]), katika ikajulika kwamba haki yakunufaika ni: “kile anachostahiki mtu kunufaika nacho, na hakuna anayemiliki kushirikiana naye katika hilo, na hili halikubali kujumuisha na badala, na inangia katika hilo mambo yafuatayo: .. Mafuta yaliyo najisi”  na Madhehebu ya Imamu Shafi yameeleza kujuzu “kuondoa kunufaika (Raaf Alyad An Ikhtisaas” katika vitu ambavyo ni najisi[3].

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Udh’hiya ni Ibada katika Ibada za kiisalamu, nayo ni katika ibada tukufu zaidi ambazo mja hujikurubisha kwazo kwa Mola wake siku ya kuchinja na masiku ya Al Tashriiq.

Damu ya Udh’hiya ni Najisi kwa makubaliano ya Wanazuoni, na ni haramu kuiuza.

Kunajuzu kuachana na damu hii na kuwapatia wenye viwanda vya mbolea kwa kupata pesa kwa njia ya “kuondoa kunufaika (Raaf Alyad An Ikhtisaas”, na hili ikithibiti manufaa yake katika kutengeneza mbolea ambayo itasaidia kukua kwa mazao, na kuthibiti kutokuwepo madhara kutokana na matumizi ya mbolea hiyo.

 

([1]) At-Tamheed, 4/44.

([2]) Al-Mandour fil Qawaaid, 3/234.

([3]) Hashiyat Al-Sharwan ala Tuhfat Al Muhtaj” 4/235-236.

Share this:

Related Fatwas