Tabia ya kuwa na ghadhabu kwa harak...

Egypt's Dar Al-Ifta

Tabia ya kuwa na ghadhabu kwa haraka na namna Sharia ya Kiislamu ilivyoikomesha

Question

Mara nyingi hunipata ghadhabu kali; hivyo hufanya baadhi ya matendo au kuchukua baadhi ya maamuzi yasiyo sahihi na yanaweza kuwa yenye athari na ya hatima, na hii huniumiza sana, hivyo nataraji kutokana na fadhila zenu kutaja baadhi ya hatua ambazo Sharia ya Kiislamu imehimiza kwa ajili ya kudhibiti ghadhabu na kuitibu, hasa na mimi ni mtu mwenye ghadhabu ya haraka

Answer

Ghadhabu ni hali inayompata binadamu mara nyingi na kumfanya atoke nje ya uvumilivu na subira, na Sharia ya Kiislamu imelaani ghadhabu na imekataza kwayo, isipokuwa ikiwa ni katika haki basi ni ya kusifiwa na yaliyo kinyume na hayo ni ya kulaaniwa kisharia, na imemwongoza Muislamu kudhibiti tabia yake kutoka kwa kauli na tendo na kutafuta msaada kwa hilo katika hali ya ghadhabu kwa hatua kadhaa kama kuzuiya hasira, na kunyamaza wakati wa ghadhabu kali, na kujikinga na Mwenyezi Mungu kutoka kwa Shetani aliyelaaniwa, na abadilishe hali yake kwa kusimama au kuketi, na vilevile kutawadha ikiwa amekasirika, na ikiwa amepata njia nyingine halali inayomsaidia kushinda ghadhabu basi hakuna ubaya nayo.

Maelezo

Hasira ni hali inayompata mtu kutokana na kuchukizwa au kukerwa na jambo fulani, hali ambayo husababisha kuchukia kitendo kilichomkasirisha na anayekifanya, au kuchukia kitendo chenyewe tu, kiasi kwamba mwenye hasira hutamani kulipiza kisasi na kuadhibu.

Hakuna tofauti ya maoni kuwa mtu anapotenda akiwa katika hali ya hasira, matendo yake hayakuwa ya kusifiwa; bali mara nyingi hufanya mambo ambayo matokeo yake si mema na baadaye huyajutia. Hasira inafanana na moto unaowaka ndani ya mwili, unaomnyang’anya mtu uwezo wa kujitawala na kumfanya apoteze mwelekeo wa fikra na vitendo vyake. Maana hii imepokelewa kutoka kwa Mtume (S.A.W).

kwani kutoka kwa Abu Sa'id Al-Khudri (R.A.) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) alisema: “Hakika hasira ni cheche katika moyo wa mwana wa Adamu, je, hamkuona wekundu wa macho yake na uvimbe wa mishipa yake?”. Imepokelewa na At-Tirmidhi katika "Sunan" yake na Al-Bayhaqi katika "Shu'ab Al-Iman".

Na kwa kuwa hasira mara nyingi humvua mtu akili yake timamu na uongofu wa maamuzi yake, kwa kutofautiana viwango vyake, basi Sharia Tukufu imekuja kuikataza na kuonya dhidi yake, ili kulinda nafsi, akili, na dini.

Hivyo, imepokelewa kutoka kwa Mu‘āwiyah bin Ḥaydah  R.A alisema: Mtume (S.A.W.) alisema: “Ee Mu'awiyah: Jiepushe na hasira, kwani hasira inaharibu imani kama vile juisi ya mti mchungu inavyoharibu asali”. Imepokelewa na At-Tabarani katika "Al-Mu'jam Al-Kabir" na Al-Bayhaqi katika "Shu'ab Al-Iman"; na (As-Sabr) ni juisi ya mti mchungu, na maana ya Hadithi ni kwamba hasira inaharibu ukamilifu wa imani na wema wote kama vile juisi ya mti mchungu inavyoharibu asali na kuiondoa faida yake kwa kupotea utamu wake, na kwa hatari ya yale yanayotokana na hasira, na yale ambayo inaweza kumfikisha mwenyewe, hasira kwa asili imekatazwa kisharia.

Na lilikuja katazo la hasira waziwazi bila mfano katika yaliyosimuliwa kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A.) kwamba mtu mmoja alimwambia Mtume (S.A.W.): “Nishauri, akasema: Usikasirikie, akarejea mara kadhaa, akasema: Usikasirikie”. Imepokelewa na Al-Bukhari katika "Sahih" yake.

Na Sharia takatifu imebainisha kwamba hasira katika baadhi ya hali inahitajika na inasifiwa kisharia, na hiyo ni pale inapotokana na kuthibitisha haki au kubatilisha batili na kadhalika. Imesimuliwa kutoka kwa Abu Ad-Darda' alisema: Nilimwuliza Mama wa Waumini Bi. Aisha (R.A.) kuhusu tabia ya Mtume (S.A.W.), akasema: “Tabia yake ilikuwa Qur'ani, anakasirikia kwa hasira yake, na anaridhia kwa radhi yake”.

Na inaeleweka kutoka humo: Kwamba hasira kati yake kuna iliyo nzuri na inayosifiwa, na kati yake kuna iliyo mbaya na inayolaaniwa, na ndiyo mahali pa katazo lililokuja katika maandiko ya kisharia.

Na kwa kuwa Sharia ya Kiislamu daima ina jitihada ya kuondoa madhara yeyote yanayoweza kumfikia mwanadamu na kumlinda asije akaangukia ndani yake, basi imeweka mkusanyiko wa njia na taratibu ambazo mtu akizizingatia huweza kujinasua na hasira, haraka yake, na athari zake. Miongoni mwa njia muhimu zaidi ni zifuatazo:

- Kuepukana na hasira na sababu zake: Na hiyo kwa kujihadhari na hasira na kujaribu kudhibiti nafsi na kuizuia ghadhabu yake, na ndiyo iliyohimizwa na Sharia takatifu, alisema Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika sifa ya waja wake wacha Mungu wanaostahiki msamaha wake: {na wanaozuilia ghadhabu} [Al-Imran: 134]; na wao ni wanaoshikilia yaliyo katika nafsi zao ya ghadhabu kwa subira, na uvumilivu hivi kwamba hasira haionekani kwao, na kwa Hadithi iliyotajwa hapo awali kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A.), katika wasia wa Nabii (S.A.W.) kwa mmoja wa masahaba wake: “Usikasirikie”.

Hadithi tukufu inaonesha kwamba kujiepusha na sababu za hasira na kutojiweka katika mazingira yanayoichochea ni mojawapo ya njia za kuikwepa hasira; kwa sababu hiyo, Sharia imeikataza. Pia imehimiza kuzizuia hisia za ghadhabu (kudhibiti hasira), kwani hilo huchukuliwa kuwa ni jitihada ya kujitawala na kujizuia kadiri inavyowezekana. Anayefanya hivyo hupata msaada wa kujikinga na hasira na sababu zake, na katika hilo kuna wokovu kwa mwanadamu duniani na Akhera.

 

Imepokelewa kutoka kwa Sahl bin Mu‘ādh, kutoka kwa baba yake, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema:
“Mwenye kuizuia hasira yake hali ya kuwa ana uwezo wa kuitekeleza, Mwenyezi Mungu huujaza moyo wake kwa amani na imani.” Imepokelewa na Abū Dāwūd katika Sunan yake na al-Bayhaqī katika Shu‘ab al-Īmān.

Na katika riwaya nyingine: “Yeyote aliyezuia ghadhabu naye ana uwezo wa kuifanya, Mwenyezi Mungu atamwita juu ya vichwa vya viumbe siku ya Qiyama mpaka Mwenyezi Mungu atamchagulia kutoka huru zenye macho mazuri atakacho”. Imepokelewa na At-Tirmidhi na Abu Dawood katika "Sunan" zao na At-Tabarani katika "Al-Mu'jam Al-Kabir".

- Kuendelea kujikinga na Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa: Kwani hiyo huondoa kwa mwanadamu kila anachokipata cha dhiki ya nafsi na hasira, alisema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na ikiwa itakushawishi Shetani kushawishi basi jikinga na Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua} [Al-A'raf: 200].

Na kutoka kwa ‘Adiy bin Thābit alisema: alitusimulia Sulaymān bin Ṣurad, akasema: Watu wawili walitukanana mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), nasi tulikuwa tumekaa pamoja naye. Mmoja wao alikuwa akimtukana mwenzake kwa hasira kali, mpaka uso wake ukawa mwekundu. Mtume (S.A.W) akasema:

“Hakika ninajua neno ambalo akilisema, yale anayoyapata yangemuondokea. Lau angesema: A‘ūdhu billāhi mina-sh-shayṭāni-r-rajīm (Najilinda kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya Shetani aliyelaaniwa).”

Wakamwambia yule mtu: “Je, husikii anachosema Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W)?” Akasema: “Mimi si mwendawazimu.” Imepokelewa na al-Bukhārī katika Ṣaḥīḥ yake.

- Kunyamaza: Kwani mwanadamu akinyamaza amejihifadhi nafsi yake kutokana na hasira, na ameisaidia nafsi yake katika kutuliza hofu, na kwa hivyo Sunna imeamrisha hivyo, kwani kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: “Mmoja wenu akikasirika basi anyamaze”. Imepokelewa na Al-Bukhari katika "Al-Adab Al-Mufrad", na Ahmad katika "Al-Musnad".

- Kutia Udhuu: Basi yeyote anayekabiliwa na kinachomkasirisha anapaswa kuchukua udhu, kwani Udhu huzima mwali wa hasira, na huondoa cheche zake, kwani kutoka kwa Abdullah bin Bujayr As-San'ani alisema: Tuliingia kwa 'Urwah bin Mohammed As-Sa'di, basi akamzungumzia mtu, akamkasirisha, akasimama akatia udhuu, akasema: Ametuhadithia baba yangu kutoka kwa babu yangu 'Atiyyah, alisema: Alisema Mtume (S.A.W.): “Hakika hasira ni kutoka kwa Shetani, na hakika Shetani aliumbwa kutokana na moto, na hakika moto huzimwa kwa maji, basi mmoja wenu akikasirika basi achukue udhu”. Imepokelewa na Abu Dawood katika "Sunan" yake na Imam Ahmad katika "Musnad" yake.

- Kumdhukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwani kumdhukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu huamsha moyoni khofu inayomsaidia mwanadamu katika adabu na kudhibiti hasira; ambapo dhikri inamsaidia mwanadamu katika kumkhofu Mwenyezi Mungu Mtukufu na ambayo inampeleka katika utiifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kisha anarudi katika adabu yake na hasira huondoka, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na mdhukure Mola wako utakaposahau} [Al-Kahf: 24]. Mwisho.

- Mtu abadilishe hali yake: Kwani katika hiyo kuna msaada kwake katika kutoka katika hali aliyo nayo, kwani kutoka kwa Abu Dharr Al-Ghifari (R.A.) alisema: Mtume (S.A.W.) alituambia: “Mmoja wenu akikasirika naye amesimama basi aketi, ikiwa hasira itaondoka kwake, na la sivyo basi alale”. Imepokelewa na Abu Dawood katika "Sunan" yake na Imam Ahmad katika "Musnad" yake.

     -Kujipamba na maadili ya kusamehe: Yule ambaye sifa hii imejikita ndani yake hadi ikawa ni tabia na mwenendo wake—yaani, huwa anawasamehe watu makosa yao—basi kuangukia katika mzunguko wa hasira kutakuwa ni jambo gumu kwake. Kwa sababu hiyo, Sharia imehimiza kujipamba na sifa ya kusamehe. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kuhusu wanaostahiki msamaha Wake: {na wanaosamehe watu} [Al - Imran: 134].

   - Uvumilivu na kutokuwa na haraka: Basi mwanadamu akikasirika anapaswa asifanye kujibu mara moja, na amudu nafsi yake, na aahirishe uamuzi wake mpaka wakati wa kuondoka hasira, basi hiyo itakuwa yenye faida zaidi kwake, kwani kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A.) alisema: Alisema Mtume (S.A.W.): “Sio hodari yule anayeshinda kwa kupindua, bali hodari ni yule anayemudu nafsi yake wakati wa hasira”. Imekubaliwa na wote.

- Mwanadamu ajue kwamba ataulizwa kuhusu kila neno wakati wa hasira: Basi anapaswa kudhibiti hisia zake ili zisimdhuru, na akumbuke kwamba Mu'min anapaswa asitoe kinywani mwake ila maneno mazuri; akifanya kulingana na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Je, huoni jinsi Allah alivyopiga mfano neno zuri kama mti mzuri mizizi yake imethibitika na matawi yake yapo mbinguni} [Ibrahim: 24], na Alisema (S.W.): {Hatoi neno ila karibu naye kuna mlinzi tayari} [Qaf: 18].

Na ikiwa mwanadamu atapata njia nyingine halali isipokuwa yaliyotajwa kati ya njia zinazomsaidia kujiondoa hasira inampasa aifanye; kwa sababu njia zina hukumu ya malengo, na kwa sababu lengo ni mwanadamu asianguke katika kinachomdhuru au kuwadhuru walio karibu naye; kwa yale yaliyothibitika kisharia kwamba hakuna kudhuru wala kudhuriana.

Na ikiwa hasira inarudiwa mara kwa mara na mwanadamu amechukua njia zote zilizotajwa na zinazofanana nazo, na hakupata mabadiliko na ikawa kwake kama ugonjwa, basi katika hali hiyo aende kwa daktari mtaalamu kutokana na uponyaji na kuchukua sababu ambazo Sharia takatifu imetuhimiza, kwani kutoka kwa Usamah bin Sharik (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: Tibianeni, enyi waja wa Mwenyezi Mungu; kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuleta ugonjwa wowote ila ameleta pamoja nao tiba.””. imepokewa na Imam Al-Bukhari katika "Al-Adab Al-Mufrad", na Ahmad katika "Al-Musnad", na wengineo.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

1 - Sharia ya Kiislamu imelaani sana hasira na ghadhabu na imeikataza, isipokuwa ikiwa ni katika haki.

2- Sharia ya Kiislamu imemwongoza yeyote anayeanguka katika hasira na inakuwa tabia inayomdhuru yeye na wengine kujiepusha nayo na sababu zake.

3- Inapasa kwa Muislamu kuchukua hatua zinazomsaidia katika kuzuia hasira, kama kujikinga na Allah kutokana na Shetani aliye mbali na rehema za Mwenyezi Mungu, na anyamaze, na achukue udhu akiwa amekasirika, na abadilishe hali yake, na ajipambe kwa tabia ya msamaha, na asiharakishe, na azuie ghadhabu yake ili aweze kudhibiti nafsi yake, na akipata njia nyingine halali inayomsaidia basi hakuna ubaya.

Share this:

Related Fatwas