Kumswalia Mtume wetu Muhammad (S.A....

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumswalia Mtume wetu Muhammad (S.A.W) kwa pamoja, kati ya rakaa za Swala ya Tarawih

Question

Ni Ipi hukumu ya kumswalia Mtume wetu Muhamad (S.A.W) kwa pamoja kati ya rakaa za Swala ya Tarawih? Na je, kufanya hivyo kunazingatiwa kuwa Bidiaa?

Answer

Kumswalia Mtume wetu Mohammad (S.A.W) ni miongoni mwa matendo mema na kunapendekezwa wakati wote. Kumswalia Mtume (S.A.W) kwa pamoja kati ya rakaa za Swala ya Tarawih huruhusiwa kisharia na inachukuliwa kuwa miongoni mwa matendo yamayopendeza.

Maelezo

Dhikri bora zaidi kuliko zote ambazo Muislamu anapaswa kuzizingatia ni kumswalia Mtume (S.A.W) kwa sababu inakusanya kati ya kumtaja Mwenyezi Mungu na kufuata amri yake ya kumswalia Mtume (S.A.W) pamoja na faida ya mema ya dunia hii na Akhera katika kumswalia Mtume (S.A.W) kama vile kuzidisha thawabu, upendo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Swala za wale wanaomswalia Mtume (S.A.W) ni utakaso wa matendo, kuinua vyeo, ​​kufikia makusudio, kutimiza mahitaji, na kupunguza dhiki. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu} [Al Ahzaab 56]

Na kutoka kwa Abu Hurairah R.A., kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema: “Yeyote atakayeniswalia mara moja, Mwenyezi Mungu atamswalia mara kumi.” [Imetolewa na Imam Muslim katika Sahih yake].

Kumswalia Mtume (S.A.W) hufuta dhambi, hutakasa matendo, na huinua cheo cha mtu.

Na dhikri kwa kumswalia Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) kwa pamoja wakati wa mapumziko kati ya rakaa za Swala ya Tarawih ni aina ya dhikri baada ya Swala, na ni wakati ambapo dua hujibiwa, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Mkisha swali basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu mkisimama, na mkikaa, na mnapo jinyoosha kwa kulala} [An Nisaa 103], Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na katika usiku pia mtakase, na baada ya kusujudu} [Qaaf 40].

Bwana wetu Abdullah bin Abbas, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, amesema: “Alimuarishe amtukuze Mwenyezi Mungu Mtukufu baada ya Swala zote,” akimaanisha kauli yake: {na baada ya kusujudu}. Imepokelewa na Al-Bukhariy katika “Al-Sahih”

Wanazuoni pia wamekubaliana kuhusu kupendeza dhikri baada ya Swala kwa ujumla, [1] iwe ni Swala ya faradhi, ya Sunna, au ya Tarawih. Amri ya kisharia ya kumdhukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumswalia Mtume (S.A.W) kumetajwa kwa ujumla, na imethibitishwa kwamba amri ya ujumla inalazimu kujumuisha nyakati, mahali, watu, na hali, kwa hivyo jambo hili ni pana ndani yake. Na Mwenyezi Mungu akiruhusu jambo kwa ujumla, basi huchukuliwa kwa maana pana, katika namna ya utekelezaji wake kwa zaidi ya njia moja, basi huchukuliwa kwa maana ya ujumla na pana, na haisihi kuiwekea mipaka kwa njia moja tu, isipokuwa kwa dalili, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi mlio amini! Mdhukuruni Mwenyezi Mungu kwawingi wa kumdhukuru. Na mtakaseni asubuhi na jioni.} [Al Ahzaab 41-42]

Hiyo ni taarifa kwa waumini, ikiwaamuru kumdhukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kutii amri hupatikana katika dhikiri ya pamoja, kama vile inavyopatikana katia dhikri ya mtu mmoja.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na isubirishe nafsi yako pamoja na wanao muomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka radhi yake} [Al Kahf 28].

Na kutii amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kujiunga na wale wanamwomba Mwenyezi Mungu hupatikana kupitia ushiriki wa pamoja katika dua, kwa kusema kwake "Amina", na kwa kuhudhuria nao tu.

Yameandikwa mengi na kuna simulizi nyingi zinazohimiza kusoma dhikri kwa sauti katika kikundi, iwe baada ya Swala au sehemu nyingine:

Ama kujuzu dhikri kwa sauti na kupendeza kwake wakati wote, imepokelewa kutoka kwa Abu Hurairah, R.A., kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, (S.A.W) amesema: kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alisema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Mimi nakuwa katika dhana ya mja wangu, na mimi niko pamoja naye anaponitajia. Akinitaja moyoni mwake, nami namtajia moyoni Mwangu, na akinitaja katika mkusanyiko, nami namtaja katika mkusanyiko bora kuliko wao, akinikaribia kwa mkono mmoja, mimi namkaribia kwa urefu wa mkono mmoja. Akinikaribia kwa urefu wa mkono mmoja, mimi namkaribia kwa urefu wa futi moja. Akinijia kwa kutembea, mimi namjia kwa mbio. Imepokelewa na Masheikh wawili.

Na Ama kujuzu dhikri kwa sauti baada ya kumalizika kwa Swala: kuna maandiko na athari yamethibitisha uhalali wa hilo. Imepokelewa kutokakwa Ibn Abbas, R.A., kwamba ameeleza: "Nilikuwa najua wanapoondoka kwa hilo (Takbira) ninapoisikia.”, imepokelewa na Bukhar na Muslim.

Pia imepokelewa kutoka kwake kwamba amesema: "Tulikuwa tukijua kuwa Mtume (S.A.W) ameamaliza Swala  kwa Takbira." Muslim katika shihi.

Na imepokelewa kutoka kwake R.A., kwamba alisema: “Tulikuwa tunajua wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alipomaliza kuswali kwa takbir (akisema 'Allahu Akbar').” Hili lilitolewa na Imam Muslim katika Sahih yake. Kutoka kwa hadithi hiyo, inaeleweka kwamba inaruhusiwa kuinua sauti ya mtu kwa dhikri na takbir baada ya Swala ya faradhi. Wanazuoni wa Madhehebu ya Hanafy wanaeleza kujuzu kumswalia Mtume wetu Mohamad (S.A.W) wakati wa vipindi kati ya rakaa za Swala ya Tarawih.[2]

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Kumswalimia Mtume (S.A.W) ni njia ya kumkaribia Mungu, kufuta dhambi, kutakasa matendo yako, na kuinua hadhi yako.

Inashauriwa kumdhukuru Mwenyezi Mungu na Kumswalia Mtume (S.A.W) baada ya Swala zote, iwe ni za faradhi au za Sunna.

Kumswalimia Mtume wetu (S.A.W) kwa pamoja kati ya rakaa katika Swala za Tarawih ni tendo linalopendekezwa kisharia.

 

[1] - Kitabu cha Al Ikaar.,( Uk.70, Ch. Dar Al Fikr).

[2] - Kitabu cha Bada’I As Swanae’ (290/10

Share this:

Related Fatwas