Kufanya kazi katika shamba la mitende kwa malipo ya asilimia ya mazao
Question
Nina shamba la mitende, na mitende hii imefikia hatua ya kuzaa. Ninakubaliana na baadhi ya wafanyakazi kwamba wailinde, waikate, waichevushe na wafanye yanayohitajika katika kuitunza msimu mzima, kwa malipo ya asilimia ya mazao yake, kwa mfano theluthi au mfano wake kulingana na makubaliano. Nini hukumu ya hilo kisheria?
Answer
Inafaa kwa mwenye shamba kukubaliana na anayefanya kazi shambani kwake kuitunza, kuikata, kuichevusha na kufanya yanayohitajika msimu mzima, kwa malipo ya asilimia inayojulikana ya mazao yake kama theluthi au kiwango walichokubaliana juu yake.
Maelezo
Kufanya kazi katika kilimo na mambo yanayohusiana nacho kama kupanda, kumwagilia, kutunza na kuangalia mazao ni miongoni mwa kazi bora kabisa zinazofanywa na watu, kwa kuwa zinatoa manufaa makubwa kwa nchi na watu wake. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu ametumia mfano wake katika kueleza fadhila za kutoa katika njia yake, kama alivyosema:
{Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu ni kama punje iliyotoa masuke saba, katika kila suke kuna punje mia moja, na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mpana na Mjuzi} [Al-Baqara: 261].
Na kutoka kwa Jābir bin ‘Abdillah (RA), kwamba Mtume (Rehma na amani zimshukie) alisema: “Muislamu hapandi mche wala hulima shamba, kisha akala binadamu au mnyama au kitu chochote, isipokuwa huwa ni sadaka kwake.” Imepokewa na Imam Muslim katika sahihi yake.
Vilevile, sheria tukufu imehalalisha mikataba na kuruhusu miamala inayokidhi mahitaji ya watu katika kubadilishana manufaa na masilahi. Miongoni mwa dalili ni kauli ya Mtume (Rehma na amani zimshukie) iliyopokewa na Ibn Hibban: katika kitabu chake kutoka kwa Jabir bin Abdallah kuwa Mtume rehma na amani zimshukie amesema “waache watu wakipeana riziki wenyewe kwa wenyewe” akimaanisha; Waacheni watu wanufaishane.
Suala hili linatathminiwa kisharia kuwa ni makubaliano ya kunyosheleza , kwa kuwa unajumuisha maana yake halisi ya kunyosheleza: Nayo ni mtu kumkabidhi mwenzake miti ili aitunzie, aiweke maji na aifanyie huduma zote, kwa malipo ya sehemu inayojulikana ya mazao yanayotokana nayo. Kwa maana hii zipo ibara na maelezo ya wanazuoni kuhusu jambi hili.
Ikiwa mtu ana shamba la mitende—kama ilivyo katika suala hili—kisha akamkabidhi mwingine kulilea kwa muda unaojulikana, kwa malipo ya asilimia ya mazao yake kama robo au theluthi, basi muamala huu unajuzu kisheria kwa kauli ya Maliki, Shafi, Hanbali, na maimamu wawili Abu Yusuf na Muhammad miongoni mwa wafuasi wa Abu Hanifa, na huu ndio msimamo wa kutoa fatwa katika madhehebu.
Inaonekana kutokana na maelezo ya wanazuoni na hukumu zao zilizokuja kuhusu kunyosheleza kuwa wamekubaliana juu ya uhalali wake hasa katika mitende - ambayo ndio suala lililoulizwa - kwani waliokubali kunyosheleza wameafikiana kuikubali katika mitende na mizabibu, kisha wakatofautiana kuhusu kuikubali katika mimea mingine ya kupandwa na mazao mengine.[1]
Asili ya uhalali wa kunywesheleza kwa malipo ya sehemu ya mazao inatokana na hadithi ya iliyopokelewa na Na`fi` kutoka kwa Ibn ‘Umar RA amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) aliwapa Mayahudi wa Khaybar kuifanyia kazi na kuilima, na kuwa wao watapata nusu ya kinachotoka humo.” Imepokewa na Bukhari na Muslim.
Kisha, pia inatilia nguvu kuainisha muamala huu kuwa ni kunyosheleza na si kukodisha; kwa kuwa hilo linachangia zaidi kupata manufaa kwa pande zote mbili, na linamfanya mfanyakazi awe na juhudi zaidi katika kutunza mti na kutozembea katika chochote kati ya hayo.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Inakubalika kisharia makubaliano kuruhusu miamala inayokidhi mahitaji ya watu kwa ajili ya kubadilishana manufaa na maslahi baina yao.
Kuainisha muamala huu kuwa ni kunyosheleza na si kukodisha; kwa kuwa hilo linachangia zaidi kupata manufaa kwa pande zote mbili, na linatia nguvu juhudi ya mfanyakazi katika kukuza mti na kutozembea katika jambo lolote la hilo.
[1] Ikhtilāf al-Fuqahā’” (ukurasa 153, chapa ya Dār al-Kutub al-‘Ilmiyyah
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
