Biashara kwa njia ya Drop Service (Huduma za Kielektroniki kupitia Wakala)
Question
Ni nini hukumu ya kutumia mfumo wa Drop Service?[1], ambapo mtu ana jukwaa la kielektroniki kuuza huduma mbalimbali za kidijitali (kama vile: miundo, matangazo, tafsiri ya moja kwa moja, picha, tafiti, programu na maendeleo, n.k.), na kufanya kama kiunganishi kati ya muuzaji - mtoa huduma - na mnunuzi - mteja - kwa kutoza kiwango cha 5% kutoka kwa muuzaji pekee? ni ipi hukumu wa kisharia katika muamala huu?
[1] Drop Service ni aina ya biashara mtandaoni ambapo mtu anauza huduma (services) kwa wateja bila yeye binafsi kutoa huduma hiyo. Badala yake, baada ya mteja kuagiza huduma, mpauzaji anawapa mtoa huduma mwingine (mfanyakazi wa tatu) ili afanye kazi hiyo, kisha anamlipisha mteja bei ya juu kulingana na faida anayotaka kupata.
Answer
Kujihusisha na biashara kupitia jukwaa la Drop Service, kwa njia ya kuwa kiunganishi kati ya muuzaji na mnunuzi, ni jambo halali kisharia, bila hofu ya dhambi, kwa sababu ni aina ya udalali unaoruhusiwa kisharia. Muunganishaji (mmiliki wa jukwaa) anastahili malipo kwa huduma anazozitoa kwa pande zote mbili kulingana na masharti yaliyokubaliwa. Kulingana na maoni ya baadhi ya Wanazuoni waliokubali, ni halali kutoza asilimia fulani ya thamani ya bidhaa; ila ni bora zaidi kubainisha malipo maalumu kwa huduma inayotolewa, ili kuepuka tofauti na kutatua hoja za utata. Hili yote lazima lifanyike kwa kuzingatia kanuni na sharia zinazodhibiti jambo hili.
Maelezo
Muamala unaojulikana kama “Drop Service” ni aina ya miamala ya kielektroniki iliyotengenezwa hivi karibuni, na kama wataalamu na watekelezaji wake walivyosema, ni kuunda jukwaa au akaunti ya kielektroniki (tovuti ya kibiashara) ambapo mmiliki wake huunda akaunti za wauzaji – watoaji huduma – kwenye jukwaa hilo, ili waweze kuonesha huduma zao za kielektroniki, na pale mteja (mnunuzi wa huduma) anapoiomba moja ya huduma hizo kwa bei iliyowekwa na muuzaji kwenye jukwaa. Muamala wa uuzaji hufanywa kati ya muuzaji na mnunuzi kupitia wakala (jukwaa), ambapo mnunuzi wa huduma analipa bei kwa jukwaa, kisha bidhaa hutumwa kwake baada ya kukamilika, na wakala (jukwaa) huchukua kiwango chake kinayokadiriwa kwa asilimia fulani ya bei ya bidhaa, kisha humtumia muuzaji salio la bei yake.
Na mtazamo wa jumla wa maana zilizotolewa kuhusu asili ya muamala huu unaonyesha kwamba unaangukia chini ya “udalali”, yaani wakala katika uuzaji na ununuzi, na anayefanya kazi hiyo huitwa “dalali”; yeye ni kiunganishi kati ya muuzaji na mnunuzi kwa malipo, na Imamu Shafi humuelezea kama “Dalali” au “muuzaji”.
Na udalali kisharia ni “wakala wa kibiashara”, na maana yake ni makubaliano ambayo dalali anahakikisha kumtafutia mtu mwingine ili kufanikisha mkataba fulani na kuwa kiunganishi katika kutekeleza mkataba huo[1].
Na dalali ni “wakala wa kibiashara”, akimaanisha kila mtu wa kiasili au wa kisharia ambaye shughuli yake, hata ikiwa ni kwa muamala mmoja tu, ni kutafuta mwenye kutaka kuingia makubaliano au kujadilian naye ili kumshawishi afunge mkataba, na vilevile kila mtu anayefanya kazi yoyote ya uwakala wa kibiashara, hata ikiwa si mara kwa kawaida na kwa mara moja tu, au akiwa na uhusiano wa kazi na mtengenezaji, muuzaji, au mgawaji kwa mkataba wa kazi[2].
. Wanazuoni wengi wa kifiqihi kutoka kwa Imamu Hanafi, Maliki, Shāfi, na Hanbali wamekubaliana juu ya uhalali wa udalali kwa ujumla, lakini walitofautiana kuhusu aina yake kwa rai mbili:
Rai ya kwanza: Inachukuliwa kuwa aina ya kukodisha, kama walivyosema wengi wa Wanachuoni wa Fiqhi kutoka kwa Imamu Hanafi, Shafi, na Hanbali. Imamu Hanafi wameweka masharti ili isihi kuwe na muda maalumu ili mkataba uwe sahihi. Wakati ambapo Imamu Shāfī na Hanbali walikubaliana ili kusihi ijulikane kazi au manufaa yanayopatikana kutokana na kazi hiyo,
Rai ya pili: Maoni mengine ni Madhehebu ya Imamu Maliki –katika kauli mashuhuri - ambapo wanachukulia udalali ni aina ya makubaliano ya kazi iliyokamilika[3].
Kwa kuzingatia maelezo ya Wanazuoni juu ya hali inayozingatiwa, hakuna kizuizi kisharia katika yale yanayofanywa na jukwaa husika kama dalali kati ya muuzaji (mtoa huduma) na mnunuzi (muhitaji wa huduma).
Ambapo muuzaji huwasilisha huduma zake kwenye jukwaa hilo, na mnunuzi hupata anachohitaji miongoni mwa huduma hizo za kidijitali kupitia jukwaa hilo pia, ambalo linachukua nafasi ya kuwa kama dalali au mshenga wa biashara. Hii hufanyika kwa malipo maalumu ambayo jukwaa linastahiki, na ambayo hukatwa kutoka kwenye bei ya huduma inayotolewa—iwe kwa mujibu wa rai ya wanazuoni wanaoichukulia kuwa ni aina ya kukodisha au kwa mujibu wa rai ya Imamu Maliki wanaoiweka katika mlango wa udalali, mradi muda umeainishwa kwa kawaida, kazi imebainishwa na kupimika, ujira umekubaliwa, na huduma inayotolewa ni halali kisheria.”
Hii ni kwa sababu imethibitishwa kisheria kwamba kubainisha ujira katika makubalioano ya udalali ni sharti la uhalali wake; kwani kutokuwepo kwa kubainisha ujira kunaleta hadaa (hatari ya udanganyifu au kutokujulikana), jambo ambalo limekatazwa kisheria. Imepokelewa na Imamu Muslim katika Sahihi yake, kutoka kwa Abu Hurayrah (RA), kwamba Mtume (S.A.W) alikataza biashara yenye hadaa.”
Na hadaa (gharar) ni jina kwa kila kitendo kilichojumuisha kutojulikana au hatari ambayo mwenye kufanya haijui, na hujificha kwake ndani yake na siri yake, na ambacho kina sura ya nje inayodanganya na ya ndani isiyojulikana. Na makusudio yake katika biashara ni: kila biashara ambayo makusudio yake hayajulikani, hayafahamiki, na hayatafikiwi wala hayawezekani.”
Na yale yaliyotajwa katika swali kuhusu kuwa wakala (jukwaa) hukata kiwango cha asilimia kutoka katika bei ya bidhaa baada ya kukubaliana hilo na muuzaji,hivyo, wanazuoni wa fiqhi wametofautiana kuhusu uhalali wake: Imamu Hanafi na Maliki – kwa kauli mashuhuri – wameona kuwa si halali, na kwamba dalali katika hali hii hastahiki ila ujira wa mfano.”
Ilhali baadhi ya wanazuoni wa Hanafi - kama Imamu Muhammad bin Salamah—na Wanazuoni wa Maliki -kwa upande usio mashuhuri - wameona kuwa mfano huu ni sahihi kwa kuzingatia haja; na uhalali wake ndiyo kauli ya Madhehebu ya Imamu Hanbali[4].”
Wala hukumu kuhusu uhalali wa kazi hii haitafautiani kwa kuwa kazi au ujira wa udalali unakatwa kutoka kwa muuzaji tu; kwani ujira wa dalali ni kwa yule aliyeemsimamia kufanya kazi hii. Ikiwa aliyempa kazi hii ni muuzaji, basi ujira wake upo kwa muuzaji; ikiwa ni mnunuzi, basi ujira wake upo kwa mnunuzi; na ikiwa ni wote wawili, basi ujira wake upo kwa wote wawili. Vinginevyo, hutatuliwa kulingana na desturi iliyo imara katika eneo hili.”
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Kuwa kufanya biashara kupitia jukwaa la Drob Service kama ilivyoelezwa ni jambo halali kisheria na si makosa, kwa kuwa linaingia katika aina ya udalali unaofaa.”
[1] Angalia: Kifungu namba (192) cha Sheria Mpya ya Biashara namba 17 ya mwaka 1999.
[2] Angalia: Kifungu cha Kwanza cha Sheria namba 120 ya mwaka 1982 kuhusu “Kurekebisha Shughuli za Uwakala wa Kibiashara na Baadhi ya Shughuli za Udalali wa Kibiashara.”
[3] Badā’i‘ al-Sanā’i‘” (Juzuu ya 4, ukurasa wa 184, toleo la Dār al-Kutub al-‘Ilmiyyah), “Rawdat al-Ṭālibīn” (Juzuu ya 5, ukurasa wa 178, toleo la al-Maktab al-Islāmī), “al-Mughnī” (Juzuu ya 5, kurasa 345–346, toleo la Maktabat al-Qāhira), “al-Mudawwana” (Juzuu ya 3, ukurasa wa 466, toleo la Dār al-Kutub al-‘Ilmiyyah)
[4] Radd al-Muḥtār” (Juzuu ya 6, ukurasa wa 63), “At-Tāj wa al-Ikhlīl” (Juzuu ya 7, ukurasa wa 499, toleo la Dār al-Kutub al-‘Ilmiyyah
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
