Ahadi ya kuuza jengo kabla ya kuimi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ahadi ya kuuza jengo kabla ya kuimiliki

Question

Kuna kijana baba yake alifariki, na akaacha duka lililokuwa limekodishwa. Kijana huyo alikubaliana na mmiliki wa duka kununua duka hilo kwa kiasi cha pesa kilicholipwa, na mauzo yalifanyika, kwa makubaliano kwamba mauzo hayo yataandikishwa rasmi na hati za umiliki kuhamishwa ndani ya wiki mbili. Wakati wa kipindi hicho, alipata mnunuzi mwingine ambaye alitaka kununua duka hilo kwa kiasi kikubwa zaidi, naye akampa ahadi ya kuliuza baada ya kumaliza taratibu za kumiliki na kuhamisha umiliki rasmi kwa ajili yake kwanza. Swali ni: nini hukumu ya ahadi hii iliyofanywa kati yake na yule aliyehitaji kununua duka hilo kisharia baada ya kumaliza taratibu hizo?

Answer

Ahadi ya mtu kuuza duka baada ya kumaliza taratibu za kumiliki kwake kwanza kwa mtu ambaye anataka kulinunua kwa kiasi kikubwa zaidi ya alichonunulia haina dosari, na ni ahadi ya kuuza ambayo inatakiwa kutimizwa na kufuatwa kisheria.

Maelezo

Sharia ya Kiislamu inaruhusu mmakubaliano yenye kuhifadhi maslahi ya pande zote mradi isiyo na udanganyifu, hadaa, madhara, riba, au vizuizi vingine. Moja ya makubaliano muhimu ni ile ya mauzo, ambayo ni kubadilishana mali au faida kwa malipo ya kudumu.

Hii inalingana na ufafanuzi wa mauzo kama ilivyoainishwa katika Sharia ya kiraia ya mwaka 1948, kifungu cha 418: "Mauzo ni makubaliano ambapo muuzaji anakubali kumhamishia mnunuzi umiliki wa kitu au haki ya kifedha kwa malipo ya pesa."

Tukitazama muamala wa swali, tunakuta kuna vipengele viwili:

Sehemu ya kwanza: Makubaliano ya mauzo kati ya pande mbili kwa duka fulani kwa bei fulani, na makubaliano ya kuandikisha mkataba huo kisharia ili kulinda haki zao na kuzuia migogoro. Pande zote ziliweka muda wa wiki mbili kumalizia taratibu. Na mradi wawili wanaofanya makubaliano wamebainisha nguzo za uuzaji na masharti yake, na wakaridhiana juu ya bei inayostahiki, na uuzaji ukafanyika kati yao, na wakakubaliana pia juu ya wakati watakaorithibitisha mkataba wa uuzaji na kukamilisha taratibu zake za kisharia, basi huo ni uuzaji sahihi unaojuzu na unaotekelezeka kisheria, na kuchelewa kuthibitisha mkataba hakuathiri usahihi wake; Muundo wa utaratibu wa hati si sharti la uhalali wa mkataba wa mauzo. wala kuchelewa kwake hakusababishi kuharibika kwa mkataba, bali mahali pa usahihi wa mkataba ni bei na kitu kinachouzwa na kukubaliana  vinavyoonyesha kupatikana kwa kuridhiana kwa wahusika wawili wa mkataba.

”Sehemu ya pili: Ni mfano wa ahadi ya kuuza, na mfano wa kuuza hutofautiana na mauzo.  Ahadi ya kuuza ni taarifa ya kupeleka manufaa siku zijazo, Kwa hivyo, ahadi tu haihusishi fidia, wala haihusishi umiliki wa kitu au manufaa.

Hivyo, kilichotokea cha kuahidiana na kukubaliana kati ya pande mbili zilizotajwa katika swali kwamba mmoja wao atamuuzia mwingine duka maalumu kwake kwa bei inayojulikana pia, pamoja na kukubaliana kwao kwamba hilo litafanyika katika wakati maalumu, na ilimradi wamebainisha nguzo za uuzaji na masharti yake ya msingi, na wakati watakaoufanya, na wakalifanya hilo kutegemea kupatikana kwa sababu ambayo ni kukamilika kwa uuzaji wa kwanza, basi jambo hilo ni halali kisharia, na ni wajibu kwa muuzaji kutekeleza ahadi hii anapomaliza taratibu za kumiliki duka hili kutoka kwa muuzaji wa kwanza.”

Hii ni kwa sababu kutekeleza ahadi ni sifa ya waumini ambao Mungu amewasifu kwa kuhifadhi amana, kutimiza ahadi na kushikamana na makubaliano. Amesema Mwenyezi Mungu: ‘Na wale ambao ni waangalifu kwa amana zao na ahadi zao.’ [Al-Mu’minūn: 8].”

Na pia kutekeleza ahadi na kushikamana na makubaliano kumejumuishwa ndani ya ujumla wa Aya nyingi zilizokuja ili kusisitiza maana ya kuitaka kutimizwa kwa ahadi na kushikamana na makubaliano, kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Enyi mlioamini! Timizeni ahadi.’ [Al-Mā’idah: 1], na kauli yake: ‘Enyi mlioamini! Mbona mnasema msiyoyafanya? Ni chukizo kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu kwamba mnasema msiyoyafanya.’ [As-Saff: 2–3].

Na imekuja katika Sunna kutoka kwa Hudhayfah bin Al-Yaman kwamba alisema: “Halikunizuia kushuhudia Badr isipokuwa kwamba mimi na baba yangu Husaīl tulitoka, na makafiri wa Quraysh wakatukamata. Wakasema: Mnataka kwenda kwa Muhammad? Tukasema: Hatumtaki, tunataka kuelekea Madina. Wakachukua kutoka kwetu ahadi ya Mwenyezi Mungu na kiapo chake kwamba tutarejea Madina na tusiondoke kupigana pamoja naye. Tukaja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) tukamjulisha habari hiyo. Akasema: Rejeeni, tuwatimizie ahadi yao, na tunamwomba Mwenyezi Mungu msaada dhidi yao.’” Ameipokea Imamu Muslim katika Sahih yake

Na katika hadithi kuna kuna dalili ya wazi juu ya wajibu wa kutekeleza ahadi.

Na Imamu Al-Qadhi Abu Bakr bin Al-‘Arabiy amepokea kutoka kwa Wanazuoni juu ya wajibu wa kutekeleza ahadi inapohusishwa na sababu miongoni mwa sababu[1]. Na juu ya hili ndipo sharia ya kiraia ya Misri katika vifungu vyake namba (101) na (102) ilipojengeka, kwani vimemweleza kuwa makubaliano baina ya pande mbili kwa kuahidiana kufunga mkataba maalumu katika siku zijazo hufungika, na huwa la lazima ikiwa mambo muhimu ya mkataba unaotakiwa kufungwa yameainishwa katika nguzo za mkataba huo na masharti yake ya msingi, ambayo hayahitaji pande mbili baada ya kuyaainisha kukubaliana juu ya jambo lolote jingine, kama kubainisha kilichouzwa, bei, na muda ambao mkataba utafanywa ndani yake, pamoja na wajibu wa kuzingatia yale yanayotakiwa na sheria katika jambo hili ya uundaji maalumu katika baadhi ya mikataba; na kwamba upande wa pili ana haki, ikiwa upande wa kwanza atajiondoa katika ahadi yake, ya kupeleka jambo hili katika mahakama, na pindi hukumu ikitoka kwa manufaa ya aliyeahidiwa ikiwa na nguvu ya jambo lililokwishahukumiwa, basi hukumu hiyo huchukua nafasi ya mkataba uliyoahidiwa.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Kutimiza ahadi ni sifa ya waumini ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasifu kwa kuhifadhi amana.

Makubaliano kati ya pande mbili kwa kuahidiana kufunga mkataba maalumu katika siku zijazo hufungika, na huwa la lazima ikiwa mambo muhimu ya mkataba unaotakiwa kufungwa yameainishwa katika nguzo za mkataba huo na masharti yake ya msingi.

 

[1] Aḥkām al-Qur'ān” (Juzuu ya 4, ukurasa wa 242, toleo la Dār al-Kutub al-‘Ilmiyyah).

Share this:

Related Fatwas