Kuingia mkataba wa kuuza matunda kw...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuingia mkataba wa kuuza matunda kwa muda wa miaka miwili, Pamoja na mnunuzi kubeba ghrama (za shamba)

Question

Nimeuza shamba langu la Maembe, kwa kiasi fulani cha pesa kwa muda wa miaka miaka miwili, baada ya makubaliano, kuna mtu akanijuza kuwa mkataba huu ni haramu; kwa madai ya kuwa nimeuza matunda ya mwaka unaofuata, pamoja na kujua kwamba mnunuzi atagharamia gharama zote, kipindi chote cha muda wa mkataba, je hukumu ya mauzo haya nini?

Answer

Kuingia mkataba wa kununua matunda kwa muda wa miaka miwili pamoja na mnunuzi kubeba gharama, hakuna ubaya kisharia, miamala hii inawekwa katika mambo ya kukodisha aradhi na kilichomo katika ardhi hiyo katika miti ili kunufaika na matunda yake.

Maelezo

Sharia tukufu imeweka vidhibiti na kanuni ambazo zinapangilia mahusiano kati ya watu wenyewe kwa wenyewe katika kuuza na kununua, kuchukua na kutoa, na ikaelekeza njia za chumo la halali katika hilo, na ikakataza yale yanayokwenda kinyume na hilo; ili kuchunga haki, kufikia masilahi na kuondoa kudhulumiana, Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: “Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhuluma, isipo kuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe.” [An-Nisaa: 29].

Muamala uliolizwa hapa unasihi kwa njia ya kuwa katika sehemu ya kukodi ardhi na kilichomo ndani yake katika miti ili kunufaika na matunda yake, na dalili ya hilo ni kitendo cha Amiri wa Waumini Omar bn Khatab R.A. katika Hadithi iliyopokelewa na Muhammad bin Al Munkadir amesema: “Asyad bin Hudhayr alifariki, na aliweka rehani mali yake kwa deni lake, taarifa ikamfikia Omar R.A. akairudisha, akaiuza miaka mitatu mfululizo, akalipa deni lake” imetolewa na Al Hafidh Abu Naeem katika Maarifa Al Sahaba, na Ameitoa Bukhary katika Al Taarikh Al Awsat, kutoka kwa Ibnu Omar R.A.: “kwamba Asyad bin Hudhayr alipofariki alimwambia mlipaji wake…..” akaitaja kwa muhtasari kama hivi.

Na imekuja katika Assad Al Ghaba  ya Ibnu Katheer katika Turjama ya Asyad bin Hudhayr R.A.: “Na akamuachia Usia Omar, Omar akaangalia wasia wake, akakuta dinar elfu nne, akauza tende zake miaka minne kwa dinari elfu nne na akalipa deni.

Katika riwaya ya Muhammad bin Munkadir “Asyad bin Hudhayr R.A. alifariki akiwa na deni la Dirham elfu sita, Omar bin Khatab akawaita walipaji wake akawapa shamba lake kwa miezi kadhaa likiwa na mitende na miti” imetolewa na Hafidh Ibnu Katheer katika Al Musnad al Farouq kutoka kwa Harb bin Ismail Alkirmany amepokea kutoka kwa Saeed bin Mansour, Uqyba amesema: “Hii ni Isnad nzuri japokuwa ndani yake kuna kukatika.

Amiri wa Waumini Omar bin Al-Khattab amefanya hivyo hali yakuwa yupo Madina akishudiwa na watu wa Makka na Madina, na haikunukuliwa kuwa yeyote kati yao alikemea hilo, na suala hili lipo katika dhana ya umaarufu”.

Na kauli ya kujuzu kukodisha mti pekee ili kunufaika na matunda yake ya baadaye, imeelezwa na madhehbu ya Hanbali katika njia mbili wameziunga mkoni Ibnu Uqyl na wengineo, na Ibnu Qayyim ameinasibisha kwa imamu Al llithy bin Saad.

Na wametolea dalili kitendao cha Amiri wa Waumini kilichotangulia, kama walivyotolea dalili juu ya kujuzu kukodisha miti ili kunufaika na matunda yake kwa kulinganisha na kujuzu kukodi ardhi ili kunufaika na mazao yake; jamhuri ya Wanazuoni wa Fiqhi wamekubaliana juu ya uhalali wa kukodi ardhi, na Imamu ibnu Al Mundhir ameelezea makubaliano hayo, na kukodi katika suala letu kunakuwa kwa badala ya kitu, ambacho ni matunda, na inajulikana kwamba kukodisha kunakuwa kwa mukabala wa manufaa; na hii kwa sababu vitu ambavyo vinakuwa kidogokidogo pamoja na kusalia asili ya mti ni kama manufaa ya kupata faida, na hili ndilo walipitisha Imamu Badr Ad-Din Al Ayny Al Hanafy.

Kama alivyonukuu Mwanazuoni mkubwa Ibnu Rushd Al Maliky kutoka kwa Imamu Abu Bakar Al Abhary kusihi kukodisha vitu kwa ajili ya kunufaika navyo pamoja na kubaki kitu chenyewe, jambo ambalo linalinganishwa na kunufaika na matunda ya mti Pamoja na kusalia asili yake.

Pia japokuwa kukodisha ardhi na mti kwa ni vitu vinavyofuatana, au mti na matunda vitu vinavyofuatana, kwani imepitishwa katika kanuni za Kifiqhi kwamba kunajuzu katika vinavyofuata yale ambayo hayajuzu katika vitu vinayofuatwa, na hili ndilo lililoelezwa na Wanazuoni wa Fiqhi kwa kauli yao: kunasamehewa katika vinavyofata yasiyosamehewa katika vinginevyo” au kunasamehe katika kitu cha pamoja yasiyosamehewa chenyewe”.

Na kukiri kwa asili hii Wanazuoni wa Fiqhi wamejuzisha kuuza vile ambavyo havijuzu kuuza peke yao bali vimajuzu kuuzwa kwa pamoja, mfano wa hilo kuuza mmea kabla ya kukomaa katika ardhi, na kuuza matunda kabla ya kuiva na mfano wake.

Wala hakudhuru katika kusihi miamala hii kuwa matunda yapo katika milki ya muuzaji; kwa sababu anaacha kilichopo kati yake na mnunuzi, na jamhuri ya Wanazuoni wanaona kwamba kukabidhi mazao au matunda kuna kuwa kwa muuzaji kumuachia mnunuzi.

Katika hili pia kunaongezwa kwamba akikubali kuingia mkataba wa kudhihiri matunda katika mti, hasa mwaka wa kwanza, sawasawa yaliyanza kudhihiri kufaa kwake au hayakuanza, basi hilo haliathiri katika kusihi kwa mkataba, kwani ikiwa matunda yamedhihiri juu ya mti, basi ima yawe yameanza kudhirhi kufaa kwake au hakukuanza, na hali zote katika hali hizi zina aina yake maalum, na hili linafuatwa katika kutofautiana hukumu za kisharia na fatwa katika hilo.

Ikiwa matunda yamedhihiri katika mti na yakaonyesha kufaa kwake, basi hilo ni sahaihi kisharia.

Ama ikiwa matunda yaliyodhihiri mwanzoni mwa kutoka kwake hayakuonyesha kufaa bado, basi hilo linajuzu kwa madhehebu ya Hanafi katika sahihi katika uhalali wa kuuza baada ya kudhihiri na kufaa pasi na sharti.

Na wamekataza kabla ya kudhihiri matunda kwa Hadithi ambayo imetolewa na Bukhari na Muslim kutoka kwa Abdullah bin Umar: Kwamba Mtume S.A.W. amekataza kuuza matunda kabla ya kudhiri kufaa kwake, na amekataza kwa muuzaji na mnunuzi” kwa sharti ya kuyaacha juu ya mti, na kwa baada ya kudhihiri kwake kwa sharti ya kukata, na hili halina kipingamizi katika kukataza.

Na inabainika kwamba madhehebu ya Abu Hanifa katika Sahihi wameshartiza ili kujuzu aina hii sharti mbili:

Kwanza: Kuwa kuuza ni huru bila ya sharti, muuzaji asiweke sharti kwa mnunuzi kukata matunda wakati wa kununua, na mnunuzi asiweke sharti kwa muuzaji kuacha matunda katika mti mpaka yaive kikamilifu.

Sharti ya pili: Kuwa matunda yananufaisha kwa sasa na baadaye, sawasawa katika kula au chakula cha wanyama au mengineyo, mpaka iaminike kuwa ni mali yenye thamani.

Mashati haya mawili yanapatikana katika masuala yetu, makataba kati ya mnunuzi na mwenye shamba upo katika matunda yenye manufaa, na imekuja moja kwa moja katika kuhusisha matunda pasi na kuweka sharti ya kuyakata sasa hivi, wala kuyaacha yaive kikamilifu, shamba na kinachopatikana ni katika milki ya mnunuzi baada ya kukabidhiwa na mmiliki wake.

Pakisemwa: Hakika muamala huu katika njia hii kunaweza kukutana mikataba miwili, nayo ni mkataba wa kukodi na kuuza, na Sharia imekataza mauzo mawili katika uzo moja.

Tunasema kwamba si kila kukutana kwa mikataba miwili kumekatazwa kisharia, kukusanya kati ya kuuza na kukodisha katika mkataba mmoja kunajuzu kwa jamhuri ya Wanazuoni wa Fiqhi wa Madhehebu ya Hanafy, Malik na Shafiy katika Madhehebu mapya, na Hanbali katika sahihi.

Pia kusihi miamala hii kunapita katika kuzingatia desturi, na watu kufuata muamala huu katika mikataba pasi na matatizo, na katika kuwatoa watu katika desturi yao kuna ubaya na uzito, na na hili nduo waliolozingatia wahakiki wa madhehbu ya Hanafy katika kujuzu kuuza matunda ya mapeasi pale tu yanapodhihri mtini.

Katika mambo ambayo yanafaa kuwa macho nayo, ni kwamba anayekodi anaweka mkono wake kwa lengo la kupata matunda kwa kuweka amana, dhamana yake haichukiliwi pasi na kuvuka mpaka au kupetuka, katika mabo ambayo Wanazuoni wa Fiqhi wamekubaliana kwamba dhamana ya kitu cha anayekodi ipo katika alichokiweka, na kwamba anayekodisha hachukuia kilichowekwa dhamana isipokuwa anapovuka mipaka au kuvunja mipaka.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Sharia imeweka misingi na vidhibiti ambavyo vinapanga mahusiano kati ya mtu mmoja mmoja wenyewe kwa wenyewe katika kuuza na kununua, kuchukua na kutoa.

Dhamana ya kitu kilichokodishwa iko juu ya mkodishaji, na anaekondishwa habebi dhamana  isipokuwa anapopetuka mpaka au kuuvuka.

Hakuna ubaya kisharia kuingia mkataba katika matunda ya shambani kwa muda wa miaka miwili au zaidi Pamoja na mnunuzi kubeba gharama.

Share this:

Related Fatwas