Hukumu ya kuokota matunda yaliyoang...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kuokota matunda yaliyoanguka mtini bila ya ruhusa ya mmiliki wake

Question

Nilikuwa nikitembea katika njiani, nikapita katika mashamba ya matunda aina tofauti, badhi ya mashamba hayo yamezungushiwa kuta, na baadhi hayakuwa na kuta. Nilitaka kuokota matunda yaliyoanguka kwenye miti ya mashamba hayo nje ya ukuta, lakini nikajizuia kufanya hivyo kwa sababu mmiliki wa shamba hakuwepo. Je, inaruhusiwa kwangu kuokota matunda yaliyoanguka mtini bila ya idhini ya mmiliki wa shamba?

Answer

Si halali kuokota matunda ya mtu mwingine yaliyoanguka ardhini au kuchuma yaliyoko juu ya miti, iwe ndani ya bustani au nje yake, isipokuwa kwa idhini ya mmiliki wake ambayo inajulikana wazi kwa maneno au kwa dalili. Isipokuwa tu mtu aliye katika hali ya dharura kabisa, anaruhusiwa kuchukua kadiri ya kutosha kuzuia njaa yake tu, bila kubeba wala kuondoka nayo.

Maelezo

Asili ni kwamba hairuhusiwi kufaidika na mali ya mtu mwingine isipokuwa baada ya idhini ya mmiliki wake. Hii ndiyo iliyothibitishwa na Hadithi ya Mtume (S.A.W.): «Haili mali ya mtu Muislamu isipokuwa kwa moyo wake mtulivu (kwa ridhaa yake)», imepokewa na Ad-Dāraquṭnī katika Al Sunan kutoka kwa Anas bin Mālik (R.A.).

Na miti iliyopandwa ndani ya nyumba au bustani inaingia katika umoja wa Hadithi hii tukufu, kwa hivyo hairuhusiwi kufaidika nayo isipokuwa kwa idhini ya mmiliki wake. Akiruhusu ndiyo, na asiporuhusu basi hapana. Lakini wanavyuoni wa Fiqhi wana maelezo mafupi kuhusu kuokota matunda yaliyoanguka mtini katika baadhi ya hali:

Madhehebu ya Hanafy wanaona kwamba matunda yaliyoanguka yakiwa mbali na vijiji, yakiwa kwenye njia ya watu (yaani hayakuzunguushiwa ukuta wala hayamo ndani ya bustani), hairuhusiwi kuyachukua isipokuwa akijua kwamba mmiliki amewapa idhini. Akiwa ametoa idhini ndipo inaruhusiwa kuyachukua. Ama yakiwa yamezingirwa na bustani au yamo ndani ya vijiji na hayamo bustanini, na matunda hayo ni ya aina yanayobaki wala hayaharibiki kwa kukaa, basi hayachukuliwi hadi ajue idhini ya mmiliki. Lakini yakiwa ni ya aina ambayo kwa kawaida hayabaki (yanaharibika haraka), msimamo unaotegemewa ni kwamba inaruhusiwa kuyachukua isipokuwa akijua kwamba mmiliki amekataza kuchukua.[1]

Mwelekeo huu wa kifiqhi unategemea Hadithi ya Abdullāh bin Umar (R.A.) kutoka kwa Mtume (S.A.W) aliyesimama na kusema: «Asimkamue mtu maziwa ya mifugo ya mwenzake bila idhini yake. Je, mnapenda mtu yeyote aje kwenye chumba chake cha kuhifadhia chakula, avunje kabati lake na kuchukua chakula chake? Hakika maziwa ya mifugo yao ndiyo yanayowahifadhia chakula chao. Basi asikamue mtu maziwa ya mifugo ya mwenzake isipokuwa kwa idhini yake.» (Imepokelewa na Al-Bukhārī na Muslim). Kwa hivyo Hadithi hii ni ushahidi kwamba yoyote anayepita kwenye mifugo ya watu au bustani yao yenye matunda hairuhusiwi kula matunda yao wala kunywa maziwa ya kondoo wao isipokuwa kwa idhini yao, isipokuwa akiwa katika hali ya dharura, ndipo inaruhusiwa kuchukua kadiri tu ya kuondoa uhitaji.

Wafuasi  wa Madhehebu za Imamu Malik, Shafy na Hanbaly wanaona kwamba inaruhusiwa kuokota matunda ya njiani ikiwa ana dharura. Ama asipokuwa na dharura, basi haijuzu kwake kuokoa kwa mdhehebu Imamu Malik (katika moja ya kauli zao), Madhehebu ya Hnbali wanasema hairuhusiwi (katika mojawapo ya riwaya mbili).[2]

Madhehebu ya Imamu Shafi wametofautisha kati ya matunda yaliyoanguka ndani ya kuta na yaliyoanguka nje yake; ambapo wanaona kuwa matunda yaliyo ndani ya kuta: hairuhusiwi kuyachukua sawa sawa na yale yaliyoko juu ya mti, lakini yaliyo nje ya ukuta: kama si kawaida kuruhusiwa, hairuhusiwi isipokuwa kwa mwenye dharura tu, naye atachukua na kumpa mmiliki thamani yake. Ama kama kuna desturi ya kuruhusiwa (kwa kiasi kidogo kinachopuuzwa na kusamehewa), rai ilio sahihi zaidi ni kuwa inaruhusiwa kuyachukua kabisa bila masharti.

Madhehebu ya Hanbali kunajuzu kuyala matunda ya mtu mwingine yasiyozungushiwa ukuta wala yasiyo na mlinzi bila ya kuzingatia njaa au dharura, kwa sharti tu asibebe wala asichukue nyumbani. Hili ni mojawapo ya mambo yapo katika madhehebu ya Hanaabila pekee.[3]

Madhehebu ya Hnabal wameitegemea Hadithi iliyopokewa kutoka Ibn Umar (R.A.) amesema: «Atakapopita mmoja wenu kwenye bustani, basi na ale, wala asifanye khubna (asibebe).» (Imepokewa na At-Tirmidhī na Ibn Mājah katika Sunan zao). Kwa hivyo Hadithi imetoa ruhusa kwa jumla bila kuifunga na ridhaa ya mmiliki wa matunda, na imeeleweka kuwa inaruhusiwa kuchukua matunda ya mtu mwingine kabisa, awe amejua ridhaa yake au hajui.

Ushahidi huu wa Hadithi kutoka Madhehebu mbalimbali unawezekana kukusanywa pamoja; kwa kutekeleza yale ambayo wataalamu wa Usuul Al-Fiqh wamekubaliana kuwa ni wajibu wa kukusanya baina ya ushahidi zinazoonekana kuwa na mgongano iwapo inawezekana, hasa kwa kuwa Hadithi zinazokataza kuchukua matunda ya mtu mwingine zina msururu wapokezi sahihi zaidi, ama Hadithi zilizotolewa ushahidi na wale wanaoruhusu znaweza kubebwa kwa maana ya mtu aliye katika dharura na msafiri, hasa wakati wa njaa kali na uhitaji mkubwa kama ilivyokuwa mwanzoni mwa Uislamu.

Maana ya hayo ni kwamba hairuhusiwi kuchukua matunda ya mtu mwingine, na huondolewa katika  hukumu hiyo mambo mawili:

La kwanza: Wakati wa dharura ambayo haitukii mara kwa mara; kwani asili ni kutokuwepo kwake, kwa msingi wa yale wataalamu wa Usuul Al-Fiqh waliyothibitisha kuwa (jambo adimu halina hukumu).

La pili: Mmiliki wa matunda kutoa idhini, iwe kwa waziwazi (hilo halina tatizo), au kwa dalili, yaani ijulikane kuwa moyo wake unaridhia hivyo kama ilivyo desturi baina ya wakulima, ndipo inaruhusiwa kwake kuchukua kiasi kisichoshikiliwa na mzozo kikawaida. Hii inategemea yale yaliyopokewa na Al-Bukhārī na Muslim kutoka kwa Anas bin Mālik (R.A.) amesema: «Abu Talhah alikuwa ndiye Mwislamu wa Madina aliyekuwa na mali nyingi zaidi, na mali aliyoipenda zaidi kuliko zote ilikuwa bustani iliyoko Beyruhaa, iliyokuwa inatazama Msikiti, Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alikuwa akiingia ndani yake na kunywa maji yaliyokuwa ndani yake yenye ladha nzuri.» Kwa hivyo katika Hadithi hiyo kuna ushahidi kuwa kula matunda ya mtu mwingine hakuna katazo ikiwa imejulikana kuwa mmiliki anayo moyo mtulivu (anaridhia) na jambo hilo.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

- Hairuhusiwi kufaidika na mali ya mtu mwingine isipokuwa baada ya idhini ya mmiliki wake.

- Kula matunda ya mtu mwingine hakuna katazo ikiwa imejulikana kuwa mmiliki anaridhia (ana moyo mtulivu) na jambo hilo.

- Hairuhusiwi kuchukua matunda yaliyoanguka ardhini bila idhini ya mmiliki wake.

- Mtu aliye katika dharura anaruhusiwa – kinyume na kanuni ya asili – kuchukua kadiri tu ya kutosha kuzuia njaa yake na kuondoa njaa yake.

 

[1] «Radd Al-Muhtaar» (4/284, chapisho la Daar Al-Fikr).

[2] «Al-Fawaaqih Ad-Dawaanii» (2/284, chapisho la Daar Al-Fikr), «Al-Majmuu'» (9/54, chapisho la Daar Al-Fikr), «Al-Mughniy» (9/417, chapisho la Maktabah Al-Qaahirah).

[3] «Al-Insaaf» (10/377, chapisho la Daar Ihyaai At-Turaath Al-'Arabiy).

Share this:

Related Fatwas