Eda ya mwanamke aliyeachika aliyeto...

Egypt's Dar Al-Ifta

Eda ya mwanamke aliyeachika aliyetolewa mfuko wake wa Uzazi.

Question

Mwanamke ameachika baada ya kuingiliwa, anataka kujua muda wake wa kukaa eda, na ijulikane kwamba amefanyiwa upasuaji wa kutolewa mfuko wake wa uzazi, mwanamke kama huyu anakaa vipi eda?

Answer

Mwanamke aliyeachika baada ya kuingiliwa, na mfuko wake wa uzazi umetolewa sehemu yake au wote, eda yake ni miezi mitatu; kwa kuingia katika eda ya mwanamke aliyeachika aliokoma hedhi; kwa sababu yao ni moja, nayo ni kukoma kwa damu ya hedhi pamoja na kukosekana uwezekano wa kurudi tena (hedhi).

Maelezo

Eda: ni muda wa mwanamke kusubiria pale kunapotokea kuachika katika ndoa, iwe kuachana huku kwa talaka au kuvunjika kwa ndoa au kufariki mume, eda imewekwa kwa maana na hekima maalum, ikiwemo: Ibada kwa kufuata hukumu za Mwenyezi Mungu, huzuni ya kuachika, ikiwemo pia:  kutakasika mfuko wa uzazi, ikiwemo pia: Kutoa furasa katika muda wa talaka rejea wanandoa kurejeana, na mwanamke anayekaa eda katika hali zote, si hahali kwake kuolewa na mwanamume asiye mumewe au aliyemuacha mpaka imalizike eda yake kwa mume wake.

Na mfuko wa mimba: Ni nyumba ya kuhifadhi mtoto tumboni, kwa maana mimba inafungamana na sehemu hii mfungamano wa moja kwa moja, ambapo Mwenyezi Mungu Anasema: “Yeye ndiye anaye kuundeni ndani ya matumbo ya wazazi kwa namna apendayo Hapana mungu ila Yeye, Mwenye nguvu na Mwenye hikima” [Aal- Imran: 6].

Na operesheni ya kutoa mfuko wa uzazi (Hysterectomy) ipo aina tatu: Kuondoa sehemu yake, na kuondo wote, aina ya tatu kuondo kila kitu katika mji wa mimba, na katika hali zote za kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mfuko wa uzazi kunapelekea kukatika damu ya hedhi kwa mwanamke moja kwa moja, na hii ni kutokana na kukosekana mji wa mimba ambao hutoa damu ya hedhi kila mwezi.

Na ikijulikana hilo: basi hukumu ya mwanamke aliyetolewa mfuko wa uzazi sehemu yake au wote, anachukua hukumu ya mwanamke aliyekoma hedhi moja kwa moja, kwa kuwa inajumuisha kukatika hedhi kwa Pamoja, kwa upande mwingine kutokuwa na uwezo kutoa mayai na yale yanayopelekea kushuka kwa damu ya hedhi, ambapo sayansi ya upasuaji wa mfuko wa uzazi imathibitisha kwamna mfuko wa uzazi unakauka baada ya kufikia umri wa kukoma hedhi na wala hawezi kuzalisha mayai katika umri huu.

Wanazuoni wamekubaliana kwamba eda ya mwanamke aliyekoma hedhi ni miezi mitatu, kwani Mwenye Mungu Anasema: “Na wale walio sita hedhi miongoni mwa wanawake wenu, ikiwa mnayo shaka, basi muda wa eda yao ni miezi mitatu”[Al Talaq: 4].

Ikisemwa: kwa nini mmesema akae eda miezi mitatu kama mwanamke aliyekoma hedhi, na akai eda kama mwanamke mwenye shaka au yule ambae twahara yake inaendelea? Kwani hedhi yake imekatika baada ya kuona damu na kabla ya kufikia umri wa kukoma hedhi.

Tunasema kwamba: kukatika damu ya hedhi kwa mwanamke mwenye shaka au yule ambae twahara yake inaendela, ni jambo la dharura na haijulikani muda gani itarudi hedhi yake, inaweza kurudi ghafla wakati wowote, tofauti na mwanamke aliyetolewa mfuko wa uzazi, kukatika hedhi kwake ni kwa kudumu na endelevu kama wanavyothibitisha wataalamu. Na tuliyopitisha katika kuungana  na mwanamke aliyekoma hedhi kunaendana na yale yaliyochukuliwa na kundi kubwa la wa hakiki wa madhehebu ya Imamu Al Zarkashy katika wafuasi wa Madhehebu ya Imamu Shafi, na Shekhe Ibnu Taymia katika wafusi wa madhehebu ya Imamu Hanbal; ambapo wanamuunganisha mwanamke aliyekoma hedhi na mwana mke mwenye shaka ambaye damu yake imekatika baada ya kuiona,  kabla ya kufikia umri wa kukoma hedhi, na kumjumuisha alietolewa mfuko wa uzazi na aliyekoma hedhi ni sawasawa zaidi([1]).

Kukisemwa kwamba damu ya hedhi inafungamana na eneo la mayai, kwani imethibiti kitaaalamu, kwamba inazuka kikawaida mpaka katika eneo la mayai.

Tutajibu kuwa sehemu ya hedhi ni mfuko wa mimba na umeondolewa kwa upasuaji, hivyo eneo inayotarajia kushuka damu ya hedhi imeondoka na haitarajiwi kurudi tena, na Wanazuoni wa Fiqhi wameeleza kuwa hukumu ya kisharia lazima ifungamane na sehemu yenyewe, na wemeelezea hilo kwa maelezo tofauti, kama vile “Kuondoa sehemu” “kutoka sehemu” “kutoweka kwa sehemu” “Kuharibika sehemu”. Sehemu ya hedhi inaondoka kwa sababu ya kuondolewa mfuko wa uzazi, kwa kuwa kweke kunatakasa mimba pasi na twahara, ikaingia katika hilo maana ya kutolewa mfuko wake wa uzazi na kuchukua hukumu ya mwanamke aliyekoma hedhi.

Pamoja na kwamba halilazimu katika hilo kuwa damu ianyoshuka katika hali ya kutolewa mfuko kuwa ni damu ya hedhi, japo kuwa kidhahiri damu inajitenga na sehemu hiyo; kwa sababu damu hiyo inaweza kuwa damu ya ugonjwa au damu inayotolewa na uchafu wa ukeni, na Sharia imethibitisha kwamba damu ya hedhi ni damu ya kawaida na inatoka sehemu ya ndani ya mfuko wa uzazi wa mwanamke, kipindi cha uzima na hali ya kawaida kama walivyoeleza Wanazuoni wa Fiqhi, kama ilivyothibitisha sayansi ya upasuaji kwamba damu ya hedhi inaitwa damu ya muda maalum ambayo inachanganyika na seli zilizochakaa, zinazoanguka katika utando wa kamasikamsi ndani ya mfuko wa uzazi.

Pakisemwa: Ipi faida ya eda kwa mwanamke alietolewa mfuko wa uzazi, ikiwa hana sehemu ya kushuka damu ya hedhi kabisa?

Tutasema kwamba: Sheria imeweka wajibu wa kukaa eda baaada ya kupatikana sababu yake ya moja kwa moja, na hii ni kwa ajili ya kutekeleza upande wa ibada, na hilo ndio lengo linalochungwa katika hukumu ya eda. Na kinachozingatiwa hapa ni hali ya anayekaa eda si kawaida ya wanawake, na dalili ya hilo: ni kwamba lau kama akifika umri wa kukoma hedhi, na akawa anatoka hedhi, basi eda yake itazingatia hali yake, hivyohivyo ikiwa hatoki hedhi katika umri ambao wanawake wanatoka hedhi, kutapasa kukaa eda kwa miezi ya kuzingatiwa hali yake.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Kwamba eda ya mwanamke aliyeachika baada ya kuingiliwa, na mfuko wake wa uzazi umetolewa, ni miezi mitatu; inaingia katika eda ya mwanamke aliyekoma hedhi; kwa sababu sababu yao ni moja, nayo ni kukatika damu hedhi Pamoja na kutokuwepo matarajio ya kutoka tena hedhi  kwa mara nyingine.

 

([1]) Nihayat Al Muhtaj 9/132. Al furou 9/248.

Share this:

Related Fatwas