Kukopa benki kwa ajili ya Kuhiji

Egypt's Dar Al-Ifta

Kukopa benki kwa ajili ya Kuhiji

Question

Mimi nafanya kazi katika benki, na nina wazo la kufungua akaunti ya benki inayowakopesha wanaotaka kufanya ibada ya Hijja au Umra kwa masharti maalum, na ningependa kujua yafuatayo:
1) Je, inajuzu kukopa kwa ajili ya Hijja?
2) Je, mtu katika hali hii huzingatiwa kuwa ana uwezo na inalazimika kuhiji?
3) Ni lazima kwa mtu yeyote ambaye anataka kuchukua faida ya mradi huu ashiriki katika mfuko wa akiba katika benki kwa mujibu wa masharti yafuatayo:
3/1) Kuingiza kiasi fulani cha pesa ambacho haiwezekani kukipunguza, lakini hakuna shida yoyote kukiongeza. Na anayeshiriki ana faida kama vile kupata kitabu cha cheki.
3/2) Anayeshiriki hatapata mkopo kwa ajili ya Hijja, isipokuwa awe mshindi wa bahati nasibu ya serikali, kisha awe mshindi pia bahati nasibu ya benki.
3/3) Kama atashinda atapata pesa zinazotosha kwa Hijja, au atapata pesa kidogo. Katika hali ya kwanza atapata pesa zake na anaweza kuzitumia atakavyo, Ama katika hali ya pili ana haki ya kukopa.
3/4) Ipo idhini kutoka wanaoweka pesa katika benki kwa ajili ya kuwakopesha wengine kwa sharti zilizotajwa.
3/5) Kuna dhamana ambazo benki huchukua kiwango cha chini cha mshahara wake na pawepo mtu mwengine mdhamini anayeuingiza mshahara wake benki.
3/6) Mkopo huwa unafutwa kwa kifo.
3/7) Hakuna riba juu ya mkopo, lakini kuna ada zisizokuwa na uhusiano na pesa zilizokopwa, lakini kwa ajili ya mshahara wa wafanyakazi, na kadhalika.
3/8) Yapo marupurupu kwa ajili ya anayejiunga, kama vile kupunguziwa bei za bidhaa mbali mbali na huduma za hoteli.
3/9) Kuna bima ya afya na kadhalika kwa anayetekeleza ibada ya Hijja atakapokuwepo katika ardhi takatifu ya Makkah na Madina.
 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na jamaa zake na masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu,
1) Kuhusu mkopo, asili yake ni halali. Ama kuhusu mkopaji, yeye anaruhusiwa kuazima pesa akiwa na uhakika kuwa atazirejea, kwa maana kuwa atapata pesa, na ameamua kuwa atalipa deni kwa pesa hizo. Kinyume na hivyo haruhusiwi kukopa ikiwa hana dharura. Iwapo atakuwa na dharura, basi analazimika kukopa kwa ajili ya kujiepusha na madhara. Lakini kama mkopeshaji akimkopesha mtu fulani, na akijua kwamba mkopaji hana uwezo wa kuzirejea pesa alizokopa, basi mkopeshaji si kosa kufanya hivyo; kwa sababu mkopeshaji mwenyewe alikuwa na kizuizi cha kukopesha, lakini akamsamehe mkopaji kwa kumpa pesa ingawa anajua vizuri hali yake ya umasikini.

Ibn Qudamah Al- Hanbali anasema katika kitabu cha [Al-Moghni 4/235, Ch. maktabat Al-Qahira]: "kukopa ni moja kati ya aina za kuazima, nayo ni halali kwa mujibu wa hadithi za Mtume na makubaliano ya wanavyuoni".

Bahooti Al-Hanbali anasema: [Kashaaf Al-Qinaa 3/313, Dar Al-Kutuab Al-Elmia]: "mkopo (Ni halali kwa anayekopa) na hauchukizi kwa sababu Mtume S.A.W. alikopa. Kama mkopo ungelichukiza, basi Mtume S.A.W. angekuwa mbali nao kuliko watu wote. Maana suala la mkopo halikuwa miongoni mwa masuala mabaya kwa sababu ya kuwahi kufanywa na Mtume S.A.W. na kwa sababu anauchukua mkopo kwa ajili ya manufaa, kwa hivyo unafanana na kununua kwa deni atakalodaiwa".

Ibn Hajar Al-hatimi Al- Shafei anasema katika kitabu cha [Tuhfatul Muhtaj 5/36, Ch, Dar Ihyau Al-Turath Al-Arabi: "na mkopo hupendeza ikiwa mkopaji hana dharura. Ama Akiwa na dharura mkopo utakuwa lazima, hata kama mkopeshaji hajui au hadhani kwamba mkopaji atautumia mkopo huu katika jambo la haramu, lakini akijua hivyo basi mkopo utakuwa haramu kwa mkopaji na mkopeshaji na akijua kwamba mkopaji atautumia mkopo katika jambo linalochukiza, basi huchukiza. Na ni haramu kukopa kwa asiye na dharura ambaye hatarajiwi kulipa deni pindipo akipata pesa kutoka upande maalum, na wakati wa kulipa deni lililocheleweshwa iwapo mkopeshaji hajui hali ya mkopaji".

2) Ama kuhusu suala la anayekopa kwa ajili ya kuhiji, je kwa kukopa kwake atakuwa na uwezo na analazimika kuhiji?
Wanavyuoni wanasema kinyume cha hivyo, kwa sababu sharti la Hijja ni uwezo, basi suala hilo haliingii katika msingi unaosema; jambo ambalo wajibu hautekelezeki isipokuwa kwalo, nalo ni wajibu.

Al-Shirazi Al-Shafii anasema katika kitabu cha [Al-lam-u, Uk.18, Ch. Dar Al-Kutuab Al-Elmia]: "jambo ambalo kitu kilichoamrishwa hakiwezi kutimia isipokuwa kwalo, ikiamuriwa kutenda na ikawa kitendo hicho hakijafanyika isipokuwa kwa kingine basi mimi huwa mwangalifu. Kama ikiwa sharti la kitu hicho ni kupatikana kwa kitu kingine kama uwezo wa kuhiji na fedha za Zaka, basi amri ya Hijja na Zaka haikuwa kwa kwa ajili ya kupatikana jambo hilo, kwa sababu Hijja hailazimishwi kwa asiye na uwezo, na Zaka hailazimishwi kwa asiye na pesa, kama tukimlazimisha mtu yeyote kufanya hivyo kwa ajili ya kuitekeleza amri hayo, basi tutazuia sharti, na hali hiyo hairuhusiwi. Kama ikiwa amri haina masharti, basi amri ya kufanya hivyo haiwezi kutimizwa isipokuwa papatikane jambo hilo, na mfano wake ni kama usafi kwa ajili ya sala, kwani amri ya sala ni amri ya usafi".

Ibn Qudamah Al- Hanbali anasema katika kitabu cha [Al-Mughni 3/216]: "Na hailazimishwi kuhiji kwa kufanya kitu kingine, na hatakuwa na uwezo wa kufanya hilo, kama akiwa anayefanya hivyo ni karibu au mgeni, na kama akipata safari na chakula kwa ajili ya Hijja, au akipata fedha. Kutoka kwa Al-Shafeiy kwamba: mtoto akifanya yanayomwezesha mzazi wake kuhiji, basi analazimishwa kuhiji, kwa sababu anaweza kuhiji bila kulazimishwa na chochote wala hakuna madhara yoyote yatakayomtokea, kwa hivyo analazimishwa kuhiji kama akiwa na chakula na mnyama wa kupanda. Na Mtume S.A.W. anasema: "Hijja ni kwa mwenye chakula na mnyama", kauli hiyo inamlazimisha anayehiji awe na vitu hivyo, au apate vitu hivyo, kwa dalili ya kwamba anayehiji ni mgeni hana chakula wala hana mnyama wa kupanda, wala hajui hata gharama zake, kwa hiyo halazimishwi kuhiji hata kama atafanyiwa hivyo na baba yake. Wala hatukubali kwamba anayehiji analazimika awe na chakula pamoja na mnyama, na kama tutakubali hivyo basi itabatilika hukumu ".

Al-Shirazi Al-Shafie anasema katika kitabu cha [Al-Muhadhab maa Sharheh llNawawi 7/68, Ch. Dar Al-Fikr]: "Na kama akipata pesa za kununulia chakula na mnyama wa kupanda, naye ana haja ya pesa hizo kwa ajili ya madeni, basi si lazima kuhiji, ni sawa sawa deni hilo ni la kulipwa wakati huo huo au baadaye, kwa sababu deni linalazimika kulipwa papo hapo, lakini Hijja inaruhusiwa kusubiri. Kwa hivyo deni linatangulia Hijja, na iwapo atazitumia fedha alizonazo kwa kuhiji, basi hatakuwa na fedha za kulipia deni".

Al -Nawawi anasema katika ufafanuzi wake: "Hivi ndivyo alivyozungumzia Al-Shafeiy katika kitabu chake (Al-Imlaa) na wanavyuoni wamekubaliana hivyo, lakini upo mtazamo mwengine finyu ni kwamba; kama ikiwa deni limeahirishwa mpaka arejee kutoka Hijja, basi analazimika kulipa deni hilo, anasema hivyo Al- Mawardi na Al-Mitwali na wengine na Al-Daramy, na mtazamo sahihi ni wa kwanza, na wanavyuoni wanakubaliana hivyo pia. Na wengi wanasema kwamba hakuna tofauti katika jambo hili. Wenzetu wanasema: "iwapo mkopeshaji atakuwa radhi kwa kucheleweshewa deni mpaka baada ya Hijja, basi hatalazimika kuhiji na wanavyuoni wanakubaliana wote juu ya jambo hili. wenzetu wanasema: Kama akiwa na deni –ikiwezekana kulilipa papo hapo, maana malipo hayo yafanyike wakati huo huo kwa kuwepo mwenye kukubali au awe na dalili nalo ni kama kulipwa kwa wakati huo. Ni lazima kuhiji hata kama haikuwezekana kucheleshwa au kulipwa haraka, maana deni hilo limeahirishwa kulipwa, au ni lazima kulipwa sasa hivi lakini mkopaji hana pesa, au anakataa kulipa, na mkopeshaji hana dalili yoyote, basi mkopaji hakulazimika kuhiji bila ya kutofautiana kwa wanavyuoni, kwani kama ikiwa hakulazimika kuhiji kwa ajili ya madeni, basi kulipa deni ni bora zaidi kuliko kuhiji. Na Mungu anajua".

3) suala la kutaja baadhi ya masharti katika mkataba, asili yake inajuzu ikiwa haipingani na maamuzi ya kisheria. Imesimuliwa kwamba Abu Hurayrah alisema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema S.A.W.: "inajuzu kupatanisha kati ya Waislamu, isipokuwa kupatanisha kunakohalalisha haramu, au kuharamisha halali". imepokelewa na Abu Dawood, na Ibnu Hibbaan ameisahihisha, hadithi hii ina dalili zimetajwa katika kitabu cha [Al-Talkhis Al-Habir 3/98, Ch. Mua’sasat Qortoba].

3/1) Ama kuhusu suala la sharti la kushirikiana si vibaya kufanya hivyo, sharti linajuzu kama ilivyotangulia, na tayari wanaoshirikiana wameshakubaliana kuhusu hivyo. Imesimuliwa kuwa Abu Musa amesema: "Mtume S.A.W. alisema:- "Hakika watu wa Ashaari wanapofiwa vitani, au chakula cha watoto wao kinapopungua mjini, wao hukusanya kile walichonacho katika nguo moja, kisha wakagawana katika chombo kimoja bila ya kupunjana, wao na mimi tupamoja". Hadithi hii imetolewa na Bukhari na Muslim.
Na dalili katika hadithi hii ni kwamba: inaruhusiwa kushiriki katika jambo halali ijapokuwa viwango vya malipo vinatofautiana na mgao kuwa kwa viwango vinavyofanana, na kwamba mgao huo huwa unakuwa kwa ajili ya anayeshiriki.

3/2) Kwa upande wa suala la bahati nasibu ni halali. Kuna dalili zilipokelewa na ambazo zinauonesha uhalali huo. Na hivyo ndivyo wasemavyo wanavyuoni. Mwanazuoni wa kufasiri Qur-an, Qurtubi anasema katika [tafsiri ya Qurtubi 3/44 - 4/86, Ch. Dar Al Kutub Al-Misriya]: anasema "Baadhi ya wanavyuoni wametohoa dalili kutoka katika Aya hii; {nawe hukuwa nao pale walipokuwa wakipiga kura ya nani miongoni mwao atakaemlea Maryamu, na hukuwa nao walipokuwa wakishindana} kwa ajili ya kuthibitisha kwamba kupiga kura ni asili katika sheria yetu kwa kila mtu anayetaka haki katika mgao, nayo ni Sunna kufuatana na wanavyuoni walio wengi katika viwango viwili kwa hoja; ili pawepo na uadilifu kati yao na nyoyo zao zitulizane, na dhana mbaya kutokuwepo kwa mgawaji, na wala hampendelei yeyote miongoni mwao kuliko mwenzake kama kinachogawanywa kitakuwa na mfanano, kwa kufuata Qurani na Sunna. Abu Obeid anasema: "Manabii watatu walitumia njia ya kupiga kura. Nao ni Yunus, Zakaria na Mtume Muhammad S.A.W.. Ibn Al Mundhir anasema: "matumizi ya njia ya kupiga kura ni kama Ijmaa (makubaliano ya wanavyuoni) kuhusu yanayogawanywa kati ya wanaoshirikiana, hakuna maana yoyote ya maneno ya wale wanaopinga. Imamu wa Hadithi Al-Bukhariy ametafsiri mwishoni mwa kitabu cha Ushahidi: sehemu ya kupiga kura katika migogoro na maneno ya Mwenyezi Mungu {wakitupa kalamu zao} na ametaja hadithi ya Nu'man bin Bashir: "mfano wa anayezingatia mipaka ya Mwenyezi Mungu na anayeikiuka ni kama wale watu waliopiga kura katika meli. Hadith".

3/3) Iwapo mtu atakuwa mshindi wa bahati nasibu ya serikali, aangalie akiba zake katika benki, kama pesa zitatosha kwa ajili ya kuhiji, basi vyema. Na analazimika kuhiji kufuatana na wanavyuoni wengi, na iwapo pesa alizonazo hazitoshi, basi achague kati ya kukopa na kutokopa, kufuatana na yaliyotangulia kuzungumzwa katika namba (1).

3/4) Kuna uwakala wa wanaoweka pesa katika benki ya kwamba wanaoweka pesa katika benki wanaweza kukopa lakini kwa masharti yaliyotajwa, na jambo hilo ni halali; uwakala unaruhusiwa kufuatana na makubaliano ya wanavyuoni. Ibn Qudamah Al-Hanbali anasema katika kitabu chake [Al-Mughni 5/63]: "Uwakala ni halali kufuatana na Quraani na Sunna na makubaliano ya wanavyuoni ... wanavyuoni wote wa umma wamekubaliana kwa ujumla kuwa uwakala ni halali, kwa sababu haja inalazimisha hivyo; basi haiwezekani kila mtu kufanya atakacho, na kwa sababu hii haja imepelekea hivyo".

Ibn Qudama anasema pia katika kitabu cha [Al-Mughni 5/87]: "Kila mtu ambae inajuzu kujifanyia jambo, na jambo hilo likawa linaruhusiwa uwakala, ni halali ya kuwakilishwa na mwanamume au mwanamke, muungwana au mtumwa, awe mtu huyo ni Muislamu au kafiri".

Sheikh Al-Maliki Al-Darder anasema: [Al-sharh Al-Kabir 3/377, Ch. Dar Al-fikr]: "Uwakala ni halali katika kila jambo linalokubali uwakilishi katika sheria ya kiislamu, nalo ni jambo ambalo halilazimishi kutendwa na mtu yeye mwenyewe; hivyo ina maana kwamba panaporuhusu uwakala, basi huruhusiwa uwakilishi, na pasiporuhusu uwakala, hairuhusu uwakilishi... na uamuzi wake ni uhalali".

3/5) Ama kuhusu dhamana ya deni kupitia mdhamini ni halali kwa makubaliano ya wanavyuoni. Ibn Qudama Al-Hanbali anasema katika kitabu cha [Al-Mughni, 4/400]: "Udhamini ni: kukusanya dhima ya mdhamini kwa dhima ya anayedhaminiwa katika ahadi ya haki. Basi yote yaliyo katika dhima yao yanalazimika, na inaruhusiwa kwa mwenye haki kuiomba haki yake kwa yeyote kati ya wawili hawa. Na asili katika uhalali wake inatokana na Qurani na Sunna ya Mtume S.A.W. na Ijmaa (makubaliano ya wanavyuoni).

Ama katika Quraani Mwenyezi Mungu anasema: {Na atakayeleta atapewa shehena nzima ya ngamia. Na mimi ni mdhamini wa hayo} Ibn Abbas anasema: mdhamini ni mwakilishi. Ama katika Sunna ya Mtume S.A.W., imepokelewa kuwa Mtume S.A.W. alisema: "Mdhamini analazimika kulipa deni". imepokelewa na Abu Dawuud na Tirmidhi akasema: hadithi nzuri. Amepokelea na Al-Bukhariy kutoka kwa Salama ibn Al-Akwa kuwa: "mtu aliyefariki alipelekwa kwa Mtume ili asaliwe, Mtume S.A.W. akasema: Je, ana deni? Wakasema masahaba: Ndiyo, Dinari mbili, akasema Mtume: Je, ameacha pesa kwa ajili ya kulipa deni hilo? Wakasema: la. Mtume akachelewa kumsalia mtu huyo. Akaulizwa: Kwa nini hukumsalia? Akasema: hatafaidika na sala yangu na dhima yake imekopwa; ila kama ikiwa kuna yeyote miongoni mwenu anaebeba jukumu la kumdhamini. Abu Qatada akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi nitalilipa deni lake. Mtume S.A.W. akamsalia mtu yule. Kwa jumla Waislamu wamekubaliana juu ya uhalali wa dhamana".

3/6) kusamehewa deni kwa sababu ya kifo -na hiyo kama ikiwa hana urithi- basi jambo hilo si vibaya, ama akiwa na urithi, ni lazima kulipa deni kutokana na urithi wake, lakini si vibaya kuacha kuomba kama washiriki wakikubaliana hivyo, mtu anaweza kuacha haki yake, na analazimishwa hivyo kama iwapo aliwekewa masharti na yeye akayakubali. Na dalili ya haya Imekwishaelezwa katika namba ya (3).

Sheikh Al-Darder anasema katika kitabu cha [Al-Sharh Al-Kabeir 3/411]: "Kama akimsamehe mtu kulipa deni (au akamsamehe haki zote) na ukawa msamaha huo bila mipaka kutokana na haki zake za kifedha zinazojulikana, au zisizojulikana kama amana au nyingine".

3/7) Kuchukua malipo kwa wale walio katika kazi hii ni halali; kwa sababu ni kwa mkabala wa kazi iliyo halali, na si kwa mkabala wa kukopa. Na jambo kama hili halihitaji dalili kwa kuwa linajulikana na pia lina dalili nyingi.

3/8) benki kuwapatia wateja wake wanaoshiriki, kuwapatia punguzo la bei katika manunuzi, hoteli n.k., mambo yote hayo ni halali. Na anayewakilisha anafanya jambo ambalo lina maslahi ya mteja kwa namna anavyoweza. Imepokelewa na Orwa kwamba Mtume S.A.W. alimpa dinar ili amnunulie kondoo, basi akamnunulia kondoo wawili, akauza mmoja kwa dinari moja na akaja na dinari moja na kondoo mmoja. ilihadithiwa na Bukhari.

3/9) Kuhusu bima ni halali. Wanavyuoni katika Idara ya Fatwa wametoa fatwa kwamba ni halali, na imefahimika kuwa mkataba wa mchango nao ni halali, na inajulikana kwamba inasamehewa katika michango, lakini haiwezekani kusamehewa katika biashara.

Quraafi Al-Maliki anasema katika kitabu cha [Al-Furuq 1/151, Alam Al-Kutub]: "Ya Pili, ni WEMA ambao hauna lengo la kuendeleza mali kama vile sadaka, zawadi na kusamehe, vitendo hivi havisaidii katika kuendeleza mali, bali pia havina madhara vikikosekana, kinyume cha sehemu ya kwanza (yaani biashara safi) ambayo ina lengo la kuendeleza mali, kwani mali hupotea kwa vitendo vya ujinga na udanganyifu".

Na kwa hivyo bima (iliyoulizwa katika fatwa hii) inafanana na WEMA huo.
Kutokana na hayo yaliyotangulia inadhihirika kuwa pendekezo lililokuja katika swali la fatwa halina ubaya. Kwa hivyo aliyeuliza anajibiwa kwamba yanajuzu yale yote aliyoyauliza katika fatwa hii.
 

Share this:

Related Fatwas