Nchi za Kiislamu kufunga mikataba y...

Egypt's Dar Al-Ifta

Nchi za Kiislamu kufunga mikataba ya kimataifa na nchi zisizokuwa za Kiislamu.

Question

Je, inajuzu kwa nchi ya Kiislamu kufunga mikataba ya kimataifa na nchi zisizokuwa za Kiislamu?

Answer

Hivi sasa nchi zote zinafunga mikataba ya kudumu ya amani, ili nchi moja isishambulie nchi nyingine, pamoja na kubadilishana mabalozi wa kudumu kati ya nchi hizi. Mikataba hii imekuwa ni msingi wa amani na heri ya kubadilishana manufaa katika ngazi ya mataifa na raia, pamoja na kuhisi amani kutoka watu wote kutoka nchi zote duniani.
Katika elimu ya Fiqhi ya kale, mkataba kati ya nchi za Kiislamu na nchi zingine ambazo hazifuati Uislamu, ulikuwa unajulikana kwa jina la msamiati "Muhadanah” au "Muwadaa`h” yaani maridhiano na kusitisha vita.
Kwa hiyo, misamiati "Hudnah, Muhadanah na Muwadaa`h " ina maana moja na neno mkataba, maana ambayo ni kufunga mkataba na maadui kwa ajili ya kusimamisha vita kwa muda maalumu kwa kulipa fidia au bila ya kulipa. Kama ilivyokuja katika [Albayan na Alumraaniy, 12/301, Ch. ya Dar Alminhaj, Jeddah}.
Hukumu katika suala hili ni kama ifuatavyo : inajizu kufunga mkataba wa muda au bila ya kuainisha muda na nchi zisizokuwa za Kiislamu. Dalili ya hayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu {Allah hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiokupigeni vita katika dini, na wala hawakukutoeni kutoka majumbani mwenu. Hakika Allah anapenda wafanyao uadilifu.}. [ Al-MUMTAHINAH: 8]
Dalili hii inaashiria uhalali wa kufanyiana mema na uadilifu na wasiokuwa maadui, na hii inawakusanya wale waliofunga na sisi mikataba ya amani inayojulikana katika enzi hii. Na Mwenyezi Mungu alisema: {Na kama "hao maadui" wakielekea katika amani, nawe pia ielekee na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika yeye ndiye asikiaye (na) ajuaye}. [Al-ANFAL: 61]. Maana ya wazi ya aya: wakikuita kwa ajili ya suluhu, basi itikia wito wao. Wameyasema hayo Ibn Zaid na Al-Suddiy, pia katika kitabu [Ahkaam Alquraan cha Ibn AlArabiy, 2/426, Ch. ya Dar Alkutub Alilmiyyah, Beirut].
Na Mtume S.A.W. alifunga mikataba na mayahudi baada ya kuhamia Madina, na waislamu waliifanyia kazi mikataba, mpaka pale mayahudi walipovunja mikataba, kama inavyojulikana katika Sira ya Mtume na vitabu vya historia.
Pia Mtume S.A.W. alifunga mkataba wa suluhu wa Hudaibiyyah, kutokana na mkataba huu aliweka utulivu na kusitisha uadui pamoja na Makureyshi, na akaunda urafiki na kabila si la Kiislamu nalo ni Khuzaa`h. Na ufunguzi (ukombozi) wa Makka ulikuwa kama ni utekelezaji wa mkataba huo .
Ni maarufu kuwa muda wa mkataba wa Hudaibiyyah ulikuwa miaka kumi, kwa mujibu wa pendekezo la Makureyshi, na Mtume S.A.W. aliukabali ingawa ni mrefu.
Aidha, Mtume S.A.W. alitoa habari za mkataba kati ya waislamu na warumi utakaotokea siku za usoni, na akawa kimya kuhusu mkataba huu, na hii inazingatiwa ni dalili ya Mtume kukubali mkataba huo.
Imepokelewa na Dhi Mikhmar, naye ni sahaba wa Mtume, aliyesema: nilimsikia Mtume S.A.W., akisema: "warumi watafunga mkataba wa amani nanyi, kisha mtawashambulia wakati wao ni maadui, mtashinda, mtasalimika,na mtapata ngawira, baadaye mtaondoka mpaka mkashuka katika konde yenye vilima. Na mkristo mmoja atainua msalaba, na kusema: msalaba utashinda, na mwislamu mmoja atakasirika, atamwendea mkristo, kisha atamuua. Hapo hapo warumi watavunja ahadi na watajiandaa kwa vita". [Ameipokea Abu-Dawuud, na wengineo].
Pia inajulikana kuwa Uislamu unajali kufikisha ujumbe wake kwa walimwengu wote, na Jihadi "yaani kupigana vita kwa ajili ya Dini" ni njia ya hayo. Imepokelewa kutoka kwa Ibn Al-Harith Ibn Muslim Al Tamimiy, kuwa baba yake alimhadithia kwamba Mtume S.A.W. aliwatuma katika Sarayya (ni vita vidogo ambavyo Mtume S.A.W hashiriki), tulipofika Almughaar (mahali), nilimhimiza farasi wangu mpaka nikawatangulia rafiki zangu. Hapo watu wa mtaa walitupokea kwa sauti za shangwe, niliwaambia: semeni: hakuna Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu tu mtasalimika, wakasema. Kisha rafiki zangu wakaja, wakanilaumu, wakasema: umetuzuia ngawira baada kuishika kwa mikono yetu. Baada ya kurudi kwetu, tutasimulia mkasa huu mbele ya Mtume S.A.W. Baada ya kusikia, Mtume S.A.W aliniita, akayasifu niliyoyatenda na akasema: hakika mwenyezi Mungu amekuandikia thawabu kadhaa wa kadhaa, kadiri ya idadi ya warumi. Kisha akasema Mtume S.A.W. nitakuandikia hoja na nitakuusia viongozi wa waislamu watakaokuja baada yangu, akaandika, akapiga muhuri, halafu akanipa. [Asad Alghabah fi maa`rifat Alsahabah, 1/415, Ch. ya Dar Alfikr, Bayruit].
Na hivyo ndivyo walivyofahamu viongozi waongofu. Kadhi Abdul-Jabbar anasema: "mfanyakazi mmoja wa Omar R.A. alimwandikia barua ambamo anasikitika kutokana na upungufu wa mali, na akasema: watu walisilimu na kwa sababu hiyo malipo ya Jizyah (yaani kodi inayolipwa na asiye mwislamu) yalipungua. Lakini Omar akachukizwa na udhuru huo, akamwadikia kuwa "Mwenyezi Mungu Mtukufu alimtuma Muhammad S.A.W. kama mwongozaji na si kama mkusanyaji mali. Kisha akamfuka kazi, na hakumtumia tena kikazi, kwa sababu ya huzuni yake kwa ajili ya uchache wa mali.
Pia Makhalifa wa Mtume S.A.W. walikuwa wakiwaambia wafanyakazi wao: "watunzeni watu na msikusanye mali kutoka kwao, maana Mwenyezi Mungu alitutuma kama walezi wala si wakusanyaji mali, na kama mtakusanya mali tu basi watakaoukuja baada yetu watakuwa wakusanyaji mali na si walezi, na wakifanya hivyo basi haya na uwajibikaji vitatoweka na baraka zitapungua. Kwahiyo shikamaneni na Uislamu.". [Tathbit Dalail Alnubuwah, 2/334, na Kadhi Abdul-Jabbar, Ch.ya Dar Almustafa, Shubra, Cairo].
Kundi la wataalamu walieleza kuwa muda ulioainishwa katika mkataba wa amani wa Hudaibiyyah si ruhusa, kwahiyo hautumiki kama ni kipimo, bali kinachopewa kipao mbele ni maslahi, kitu chenye maslahi kinafanyiwa kazi hata kama mkataba utakuwa zaidi ya miaka kumi.
Al Mirghinaniy katika [mlango wa mikataba ya amani na anayestahiki usalama] anasema: "Imamu akiona kufunga mkataba na maadui au kundi miongoni mwao kuna masilahi kwa waislamu, basi si kosa kufanya hivyo”, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na kama "hao maadui" wakielekea katika amani, nawe pia ielekee na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika yeye ndiye asikiaye (na) ajuaye}. [ Al-ANFAL: 61]. Pia Mtume S.A.W. aliwekeana mkataba wa amani na watu wa Makka, mwaka wa Hudaibiyyah, kwa kusimamisha vita kati yao muda wa miaka kumi. Na mkataba ni Jihadi kimaana ukiwa una manufaa kwa waislamu. Lakini mkataba ukiwa una madhara kwa waislamu, basi haujuzu".
Al Babertiy anasema katika maelezo yake "hukumu haihusishi muda uliopo katika mapokezi, nao ni miaka kumi, sababu muda huu ni kiasi tu kilichokadiriwa, kisichozuia kuongezeka au kupungua kwa muda , kwani muda wa mkataba hutokana na masilahi ya waislamu. Kwa hiyo, muda unaweza kuongezeka au kupungua". [Alinayah, Sherehe ya Alhidayah, 5/455, Ch. ya Dar Alfikr].
Abul Khattab anasema: "Maneno ya Imam Ahmad yanajuzisha mkataba wa zaidi ya miaka kumi, ikiwa kuna masilahi. Na hivyo hivyo, anasema Abu-Hanifa, kwa sababu huu ni mkataba unakubalika kuwa miaka kumi, basi inajuzu kuzidisha, kama vile mkataba wa kukodisha. Muda unaainishwa kuwa ni miaka kumi kwa ujumla ili kuwezesha kuurefusha kwa kuonyesha kuwepo lengo la kuzidisha huko, nalo ni masilahi makubwa zaidi yanayopatikana katika mkataba kuliko katika vita". [Almughny, na Ibn Qudamah, 9/296, Ch. ya Maktabat Al Qahirah].
Wapo waliosema kuwa mkataba unajuzu kuwa wazi bila ya kuainisha muda ikiwa kuna masilahi ndani yake. Ibn Taimiyyah anasema: ama kauli yake Mwenyezi Mungu{(Hili ni) tangazo la kujitoa katika dhima (ahadi), litokalo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa washirikina} kuwa mikataba kama hiyo ni ya hiari na si ya Na Mtume S.A.W. alikuwa ana hiari kuipitisha au kutoipitisha, kama vile hukumu ya "Wakala" .
Lakini, baadhi ya wanachuoni wanasema:mkataba haujuzu isipokuwa kwa muda maalumu. Kauli hii inakwenda kinyume na misingi ya Imam Ahmad, kauli yao pia inakanushwa na Quraani na Sunna. Maana Mtume S.A.W. hakuwapangia muda maalumu wengi wa aliowekeana mikataba ya amani. [Majmuu` Alfatawa, 29/140, Ch. ya Majmaa` Almalik Fahd, Madinah, Saudi Arabia].
Kwa mujibu wa yaliyotangulia: Inajuzu kwa nchi za Kiislamu kufunga mikataba ya kimataifa na nchi zisizokuwa za Kiislamu, madamu mikataba hiyo haiendi kinyume na Sheria ya Kiislamu. Sawa mikataba hiyo ni ya muda maalumu au ya wazi bila ya kuainisha muda.
Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas