Maadili ya Kiislamu na Mweleweko wa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Maadili ya Kiislamu na Mweleweko wake

Question

Ni upi mweleweko wa maadili ya Kiislamu ?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
1- Dhana ya maadili katika Uislamu –kutokana na maoni ya marehemu- profesa: Mohammad Dhiyaa Aldin Al-Kurdiy, profesa na raisi ya kitengo cha Akida ya kiislamu na falsafa -Chuo Kikuu Al-Azhar- kwamba dhana hii lazima itokane na misingi yake yenyewe iliyojengeka kwa vyanzo vyake vya asili. Kisha uislamu ni ule aliokuja nao Mtume Muhammad S.A.W na akaubainisha kwa yale aliyomteremshia Mwenyezi Mungu Mtukufu miongoni mwa maamrisho na makatazo. Na kwa ajili hii, dhana ya maadili ya kiislamu lazima ichukuliwe kutoka katika vyanzo hivyo ili iafikiane na misingi yake inayoitegemea na uasili wake, na kutokana na hayo tunaweza kusema kwamba dhana yake ni: “Kutekeleza yale aliyokuja nayo Mtume S.A.W miongoni mwa maamrisho na makatazo”, na haya ndio ukweli wa maadili ya kiislamu. Na Al-Ghazaly alisema kwamba dhana ya maadili ni: “Mfumo thabiti ambao kwayo hujitokeza vitendo kwa urahisi na wepesi bila ya kuwepo haja ya kufikiria au kuangalia. Mfumo huo utakapokuwa unatoa vitendo vizuri vinavyosifika kwa sifa njema kiakili na kisheria basi huitwa maadili mema au tabia njema. Na iwapo Mfumo huo utatoa vitendo vibaya basi huitwa mfumo huo ambao ndio chanzo, huitwa tabia mbaya”.

2- Kwa upande mwingine, kuna baadhi ya wataalamu wa falsafa ya Kiislamu walitaja baadhi ya dhana za maadili ambazo hazifai kuwa dhana za maadili ya kiislamu, miongoni mwa dhana hizo ni dhana ya Al-Faraby katika kitabu chake [Tahsil Al-Saadah] kuwa ni: “Kufanya kazi kikamilifu kwa kuelekezwa na nguvu ya kifikira”, na kwa mwelekeo huu, Ibn Maskweh aliafikiana na dhana hii katika dhana yake.

3- Na kwa upande mwingine, kwa hakika ufahamu wa maadili ya kiislamu unahusiana na chanzo au asili yake ya kheri na shari katika binadamu, na asili ya kheri katika binadamu ni roho {Sema: Roho ni jambo lililomuhusu Mola wangu (Mwenyezi Mungu}. [BANI ISRAIL 85]. Kwa hivyo kheri inatokana na roho, kwani hiyo roho ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani roho ina upole wa Mwenyezi Mungu ambao -wenyewe- huwa unaelekea katika kheri isipokuwa mwanadamu chanzo cha shari ambacho ni nafsi kitakapomtawala mwanadamu. {(Kwa hakika (kila) nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu isipokuwa ile ambayo Mola wangu ameirehemu} [YUSUF 53] .Kwa hivyo nafsi ndio chanzo cha shari kutokana na kutuama ndani yake nguvu za matamanio na hasira.
Na miongoni mwa mambo ya kushangaza ni kuwa nafsi ni siri ya maendeleo na ustawi, kama si nafsi basi pasingelikuwepo jitihada na pasingelikuwepo maendeleo. Kwa hivyo roho ni kitu kisafi na kilichotahirika sana na kinaendelea kupanda daraja kwa nmna ambayo haina mwisho. Na nafasi ni kama uzito ulio karibu na sehemu ya roho katika uongozi wake ili ichukue nafasi yake ya kawaida katika uhalisia wake, na roho zitofautiane na vyeo vikawa vinapanda juu ya vingine kwa kiasi cha kupatikana kwa uzuiaji wa nafsi inayoamuru mambo, na kuigeuza kuwa nafsi yenye kulaumu, na kuipeleka baada ya hapo ikawa nasi yenye kutulizana kwa matumaini, na kisha kwa namna aitakayo Mwenyezi Mungu kwa nafsi hiyo katika kuipandisha vyeo.

4- Na kwa mgongano huu wa daima baina ya roho ambayo ni chanzo (asili) cha kheri na nafsi ambayo ni chanzo cha shari, tunaweza kusimama katika mweleweko wa maadili ya kiislamu –huku tukizingatia ndani ya mweleweko wa malezi– kuwa ni hali ambayo roho hujaribu kuvifanya vitendo vya nafsi vitokane na mafunzo ya Mtume S.A.W pamoja na kuwa na imani nayo na matumaini. Ama tukiuchukua mweleweko wake kwa maana ya baada ya malezi na mwenendo, hivyo basi utakuwa mweleweko wake huo ni sura ya nafsi, ambayo kwayo hutokea matendo yake yanatokana na mafunzo ya utume kwa urahisi, usahili, imani na matumaini, baada ya roho kuilea na kuihamisha kwa malezi yake kutoka katika nafsi yenye kujilaumu na kuwa nafsi yenye utulivu.

5- Na lazima tunapouzungumzia mweleweko wa maadili ya kiislamu tuanze kwa kuangalia maana ya kilugha ya neno (KHOLOK) ambalo ni la kiarabu –kama anavyosema profesa Abdulhamid Madkor, mkuu wa kitengo cha falsafa ya kiislamu, Kitivo cha Dar Al-Ulum- kuwa neno hili lina maana nyingi, miongoni mwazo ni: Dini, ushujaa, tabia, ukarimu, sifa na ada. Mtu husemwa kuwa: hakika yeye ana hulka kwa maana yeye ni mwenye dini. Na miongoni mwa wanaoitumia maana hii ni swahaba Abdullahi Ibn Abbas katika tafsiri yake ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {"Hayakuwa haya (ya kuja watu wakasema kwao ni Mitume) ila ni tabia ya watu wa (tangu) kale (tangu zama za zama)"}[ASH-SHUARAA 137] yaani haikuwa hii isipokuwa ni dini ya waliotangulia. kwa hivyo maana ya hulka ya waliyotangulia ni Dini yao waliyokuwanayo, na madhehebu yao waliyoyatumia kwa mambo yao. Na ibn Abbas alifasiri pia kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na bila shaka una tabia njema kabisa}[AL QALAM 4] kwa maana hiyo hiyo, ya dini iliyo tukufu miongoni mwa dini za Mwenyezi Mungu. Jambo hilo linauthibitisha uhusiano mkubwa baina ya dini na hulka au maadili. Dini ni msaidizi mkuu aliye mpana ambaye maadili huhukua kutoka kwake yaliyo bora na yenye shani ya juu. Kwani uwanja wa dini ni mpana sana na hukusanya elementi nyingine nyingi sambamba na maadili, kama vile itikadi, hukumu za kiislamu na mifumo ya aina tofauti ambayo Uislamu huifanya kuwa katika nidhamu moja chini ya kivuli chake tena kwa thamani ya juu.
6- Ama maana ya tabia na sifa, husemwa kuwa mtu ana tabia na hulka nzuri. Na hivyo alivyo kimaumbile kwa maana kuwa ameumbiwa hivyo na imekuwa tabia yake. Na kwa ajili hii, wataalamu wa lugha wanaangalia tofauti baina ya neno la ‘kiumbe’ na la ‘huluka’ katika asili ya neno hilo la kiarabu na kukuta kuwa yana asili moja. Kwani neno kiumbe (khalq) linachukua upande wa dhahiri wa mwanadamu, na neno tabia -huluko- (khuluq) linachukua upande wa ndani ya mwanadamu. Na pande zote mbili zinaweza kusifiwa kwa sifa nyingi nzuri au mbaya, kwa wema au kwa uchafu. Na ingawa pande zote mbili za nje na ndani ya mwanadamu zina umuhimu wake, hakika upande wa hali ya mwanadamu ndio wenye umuhimu mkubwa zaidi, kwani huo ndio upande unaoungana na utashi na uchaguzi wake nao kimsingi ndio nguzo kuu ya kukirimiwa kwake na siri ya kuwa kwake na sifa ya kipekee. Na upande huu ndio wenyekustahiki kuongoza na kuutawala upande wa nje na kuwa juu yake.

7- Marejeo:
1- Prof. Mohammad dhiyaa Al-Din Al-Kurdy, Al-Akhlaq Al-Islamiah Wal-Sufiah, Al-Qahirah, Ch. Al-Saadah, 1409, H-1989 Uk. (Ku. 18-21)
2- Prof. Abdulhamid Madkur, Dersat Fiel Al-Akhlaq, Al-Qahirah, Dar Al-Hanii, 1426, H. 2005 Uk. (Ku. 9-12).
 

Share this:

Related Fatwas