Wakati wa kufuturu Mwenye Saumu kat...

Egypt's Dar Al-Ifta

Wakati wa kufuturu Mwenye Saumu katika Ndege

Question

Tulisafiri kutoka Misri hadi Canada kwa ndege ya kimisri, mwanachuoni mmoja alifutu kwa kututaka tufunge, licha ya kuwa ndege itakuwa angani kwa saa kumi na moja takriban, na tulipanda ndege saa saba mchana na tulifuturu kwa wakati wa wa Misri, lakini tatizo ni kwamba tulifuturu hali ya kuwa jua bado linawaka, na halijazama ila mwishoni mwa safari, yaani baada ya muda wa saa kumi na moja, kwa kuongezea ule wakati unaoutangulia ambao ni sehemu ya wakati wa daku. Nini fatwa ya jambo hili?

Answer

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimfikie Mtume Muhammad S.A.W., watu wake, masahaba wake na waliomfuata. Ama baada ya hayo:
Mwenyezi Mungu Mtukufu alifaradhisha Saumu juu ya waislamu, na akafafanua kuwa mwanzo wake tangu kuchomoza Alfajiri, na mwisho wake kuzama jua, alisema S.W.: {Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa Alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku.} [AL BAQARAH 187]. Na katika sahihi mbili kutoka kwa Omar Bin Al Khattaab R.A., Mtume S.A.W. alisema: "Usiku ukiingia hapa hapa, na mchana ukaondoka hapa hapa na jua likazama, basi mwenye Saumu amefuturu".
Na huvuliwa katika hayo, hali ambazo mtu anaruhusiwa kula, mwanachuoni Ibn Abdeen Al Hanafiy alizipanga kwa kusema: Mtu anaruhusiwa kula (kuacha funga) katika mambo tisa; mimba, kunyonyesha, kulazimishwa, safari, ugonjwa, jihadi, njaa, kiu na uzee. [Rad Al Mukhtaar 421/2, Ch. Dar El Kutub Al Elmiyah].
Anayesafiri safari ndefu ya halali anaruhusiwa kufuturu, Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: {Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi (atimize) hisabu (ya siku alizowacha kufunga) katika siku nyingine} [AL BAQARAH 185], Allah sw amemruhusu msafiri kufuturu kwa sharti ya kulipa baadaye siku ambazo amekula. Katika sahihi mbili kutoka kwa Aisha R.A. kwamba Hamza Bin Amro Al Aslamiy alimwambia Mtume S.A.W. "Je, iko Saumu safarini? na alikuwa anafunga sana, basi Mtume S.A.W alisema: ukitaka funga na ukitaka fungua!" Alimpa hiari kati ya kufunga na kufungua, sawa iwe Ramadhani au siku nyingine.
Na pia inajuzu kufungua kama muda wa Saumu utarefuka, na kumsababishia shida itakayopelekea madhara au kuangamia au kuharibika, na inajuzu kufungua kama njaa au kiu itamzidi kiasi ambacho anaogopea nafsi yake.
Al Kassaaniy alisema katika kitabu cha [Al Badaa'i]: " Inajuzu kufungua kama mtu anaogopa kuangamia kutokana na njaa na kiu kali, kwani hali hii ni kama ugonjwa ambapo mtu anaogopa kuangamia kama atafunga hali ya kuwa ni mgonjwa". [Al Badaa'i 97/2, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Na Al Nawawiy alisema katika kitabu cha [Al Majmou'i]: "Wenzetu na wengineo walisema: aliyezidiwa na njaa na kiu, na akaogopa kuangamia basi ni lazima kufungua, hata kama ni mzima na mwenyeji; kutokana na tamko la Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msijiue (wala msiue wenzenu). Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kukuhurumieni.} [AN NISAA 29]. Na kauli ya Allah s.w:{Wala msiitie mikono yenu katika maangamizo} [AL BAQARAH 195]. Kwa hiyo atalazimika kulipa kama mgonjwa. [Al Majmuo'i 262/6, Ch. Makatabat Al Ershaad. Jeddah].
Na kuhusu msafiri kwa ndege basi yeye anafuata hukumu iliyopita, inajuzu kufungua, ima kwa sababu ya safari au kupata shida kwa sababu ya urefu wa muda wa Saumu, basi ana haki ya kufungua pia kwa sababu ya ugumu maradufu zaidi katika safari, lakini kama atachagua kufunga basi kufuturu kwake ni kuzama kwa jua lote kwa kuhakikisha yeye mwenyewe au kuambiwa na mtu anayemwamini, na haifai kufuturu kwa kutumia majira ya nchi yake au nchi anayopita, haya ni kwa mujibu wa aya na utaratibu wa sheria ya Kiislamu. Allah s.w amesema:{Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa Alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku.} [AL BAQARAH 187].
Na inajulikana kuwa usiku hauji ila kwa kuzama jua, kama vile kila mtu anajua muda wa mwisho wa kula daku, muda wa kufuturu na nyakati za sala kutokana na sehemu ambayo yupo au anga anayopita.
Ibn Abdeen alinukuu hayo akasema: "Alisema katika Alfaidhi: Aliyopo sehemu ya juu kama vile mnara wa Alexandria hafuturu kama jua halijazama kwake, na watu wa mji huo wanafuturu kama jua litazama kwao kabla yake. Kwani mazingatio ya kuchomoza ni haki ya Sala ya Alfajiri au daku. [Rad Al Mukhtaar 420/2].
Kwa kuangalia dunia na kuzunguka kwake jua, basi jua halizami katika wakati mmoja ulimwenguni, na aliye karibu zaidi na dunia basi jua huzama kwake kabla ya aliye mbali na dunia. Kwa hiyo kila mmoja kati yao analazimika kufuturu jua linapozama hata kama aliye karibu amefuturu kabla ya aliye mbali.
Na Al Zelaiy alisema katika kitabu cha [Tabiyen Al Haqaiq]: "Na anayeona mwandamo wa mwezi wa Ramadhani au fitri, kauli yake ikapingwa, basi yeye anafunga". Al Shalabiy alisema katika hayo: Kauli yake “kauli yake ikapingwa”, yaani imepingwa kwa sababu ya tuhuma ya ubaya kama vile mawingu yana ila, au kwa kuwa ameona peke yake, hata kama ni mwadilifu. Na katika kitabu cha [Al Mabsuott]: Imamu anakataa ushahidi wake kama mawingu yako safi na yeye ni miongoni mwa watu wa mji, lakini kama mawingu hayako safi au alikuja kutoka nje ya mji akitokea sehemu yenye muiniko, basi ushahidi wake unakubaliwa. [Al Mabsuott 318/1 Ch. Dar Al Kitaab Al Islamiy].
Na alivua hali mbili katika kutokubaliwa ushahidi wa mwandamo, ikiwemo muiniko wa sehemu aliyoonea shahidi, kwani ameifanya sehemu iliyoinuka ndio sababu ya kukubaliwa ushahidi wake, kwa sababu kuona kwa kupitia sehemu iliyoinuka ni tofauti na sehemu ya chini.
Na alisema katika kitabu cha [Majma'a Al Anhar]: "Altahawiy alisema: inatosha shahidi mmoja -yaani katika kuthibitisha mwandamo- kama alikuja kutoka nje ya mji au alikuwa juu ya mahali pa juu” .. kwa hitilafu ya kuchomoza na kuzama kutokana na hitilafu ya sehemu iliyoinuka au iliyo chini. [Majma'a Al Anhar 337/1, Ch, Dar Ihiyaa Al Yuraath Al Arabiy- Bairut].
Na kama msafiri kwa ndege amehakikisha kuzama kwa jua akafuturu kisha jua likadhahiri tena basi Saumu yake ni sahihi, na hana kosa kwani alifuturu kwa kutegemea dalili ya kisheria, kwani mazingatio -kama ilivyopita- katika kufuturu ni kuhakikisha kuzama kwa jua, na jua likizama kwa elimu wake au kwa kuambiwa na anayemwamini, basi halazimiki kujizuia kula. Ama akifuturu kwa kudhania kuwa jua limezama ilhali halikuzama, basi lazima alipe funga. Katika sahihi ya Bukhaariy kutoka hadithi ya Asmaa Bint Abu Bakar, alisema: “Tulifuturu katika zama ya Mtume S.A.W. katika siku yenye mawingu, kisha jua likachomoza, Hishaam aliambiwa: J walilazimishwa kulipa? alisema: lazima kulipa”.
Na kama mawingu yametanda ambapo ni vigumu kuona jua basi hafuturu isipokuwa kwa yakini, lakini muda wa Saumu ukirefuka na akapata shida basi ana haki ya kufuturu kama ilivyopita.
Kutokana na hayo yaliyotangulia: kwa mujibu wa swali; Inajuzu kufuturu katika safari iliyotajwa na mabayo ni kwa ndege, kwa kuwa imekamilisha masharti ya safari yanayoruhusu kufutu, na kama msafiri ataamua kufunga basi anafuturu kwa kuhakikisha kwamba jua limezama hata kwa muda mdogo sana katika anga ya ndege, na kama Jua litarejea tena basi asilitazame, au aliambiwa hivyo na mtu anayetegemewa kwa kuwa kwake mkweli. Na kama si hivyo basi iwapo muda wa Saumu utakuwa mrefu zaidi basi ana haki ya kufuturu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi ya wote
 

Share this:

Related Fatwas