Sifa Kuu za Maadili katika Uislamu.
Question
Ni Sifa kuu gani muhimu za maadili katika Uislamu ?
Answer
Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimfikie Mtume Muhammad S.A.W., watu wake, masahaba wake na waliomfuata. Ama baada ya hayo:
Kwa hakika upande wa kimaadili katika Uislamu ni mfano mzuri kwa ubinadamu kuliko nadharia na falsafa zote duniani ,na sifa muhimu za upande wa kimaadili katika Uislamu ni kama ifuatayo :
1- Akida katika Uislamu ni chimbuko la maadili, na juu ya misingi ya Akida hupatikana jambo la mwafaka wa kinafsi na utulivu wa kindani kwa nafsi ya kibinadamu. Kwa hakika upweke wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika dhati, sifa na matendo ni kiini cha Akida, kwani mitazamo na itikadi sahihi katika ulimwengu, binadamu na maisha ni njia ya ujenzi wa jamii na furaha ya watu wake.
2- Upande wa kimaadili katika Uislamu unasisitiza juu ya athari ya Akida katika utulivu wa kimoyo, na umepiga mfano mzuri sana katika jambo hilo. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Mwenyezi Mungu anakupigeni mfano wa mtu mwenye mabwana washirika wanaogombana, na wa mtu (mwengine) aliyehusika na bwana mmoja tu. Je! Wako sawa katika hali zao? Alhamdu lillahi, Lakini wengi wao hawajui. Basi shughulika na bwana wako mmoja tu Mwenyezi Mungu} [AZ ZUMAR 29].
Na katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na anayemuamini Mwenyezi Mungu huuongoza moyo wake (kwendea maliwaza mazuri). Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.} [AT-TAGHABUN 11].
3- Katika Uislamu ibada zimewekwa kwa ajili ya kutakasa utukufu wa kiroho, na maumbile ya Malaika katika binadamu, na kumwepusha binadamu kutokana na matamanio ya nafsi. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema kuhusu Sala:{Soma uliyofunuliwa katika kitabu na usimamishe Sala. Bila shaka Sala (ikisaliwa vilivyo) humzuiliya (huyo mwenye kusali na) mambo machafu na maovu, na kwa yakini kumbuko la Mwenyezi Mungu (lililomo ndani ya Sala) Ni jambo kubwa kabisa (la kumzuilia mtu na mabaya). Na Mwenyezi Mungu Anajua mnayoyatenda.} [AL-ANKABUUT 45).
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kuhusu Zaka: {Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (sadaka zao) na kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaombee dua. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu (watengenekewe) na Mwenyezi Mungu ndiye asikiaye na ajuaye.} [AT-TAWBA 103).
Na katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu Hija: {Hija ni miezi maalumu. Na anayekusudia kufanya Hija katika (miezi) hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika hiyo Hija. Na kheri yoyote mnayoifanya, Mwenyezi Mungu huijua. Na jitengezeeni zawadi. Na hakika bora ya zawadi ni ucha mungu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili!.} [AL-BAQARAH 197).
4- Miamala baina ya watu ni kiini cha tanzu zote za imani, na anwani yake kuu ni wema na Taqwa. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na saidianeni katika wema na Taqwa, wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu; Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.} [AL-MAIDAH 2].
5- Nguvu ya kibinadamu huelekezwa katika kufanya kheri kifikra, kihisia na kitabia, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Enyi mlioamini! rukuuni na sujuduni na mwabuduni Mola wenu na fanyeni mema, ili mpate kufaulu.} [AL-HAJJ 77].
6- Misingi ya mahusiano baina ya watu katika Uislamu huwa kwa upendo na undugu kama vile ni kutoka familia moja. Mtume S.A.W. anasema: "Tahadharini na dhana, hakika ya dhana ni habari za uongo, wala msichunguzane, wala msipelelezane, wala msifanyiane ghushi katika biashara, wala msifanyiane husda, wala msipeane mgongo bali kuweni waja wa Mwenyezi Mungu kama ndugu". [Al Bukhariy "5719" na Muslim "2563" Kutoka kwa Abu Hurayrah].
7- Kwa kweli, jamii yaweza kulaumiwa kwa maadili yake kama mtu. Na kiutu haiwezekani kupata mafanikio kama hakuna kigezo kizuri cha kuiga. Na kiutu inatakikana kufikia kigezo hiki kizazi baada ya kizazi. Na haiwezekani kufikia ila kwa kupitia wahyi sahihi wa Mwenyezi Mungu ambao ni Quraani Tukufu na Sunna ya Mtume S.A.W.
8- Maadili katika Uislamu hayasifu yasiyokuwa hayo kwamba ni maadili ya Kiislamu tu, bali je maadili ya nguvu? Je maadili ya mapenzi? Je maadili ya kijamii? Je maadili ya kibinadamu? Baadhi ya wakati yako hivyo lakini sio hivyo kila wakati, kwani Uislamu unasifu baadhi ya maadili hayo na kuyakosoa baadhi yake hasa madhehebu ya wanafalsafa ya nguvu. Na baadhi ya tabia zinasifiwa na Uislamu kwamba ni tabia za kimapenzi lakini Uislamu unakemea anayependa uchafu na unapongeza anayependa mazuri.
9- Si misingi yote ya tabia katika Uislamu inakuwa katika uwastani au hali ya katikati kama yanavyosema madhehebu ya kigiriki na falsafa nyingine. Bali kuna tabia zinaruhusu binadamu atoe juhudu kubwa ili kufikia katika daraja ya juu zaidi na si kutosheka katika kikomo cha wastani, kwa mfano kufanya mambo ya kheri kiujumla hakulazimishi kufikia katika kikomo cha wastani. Na Allah S.W. ameashiria hayo katika kauli yake: {Enyi mlioamini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni macho, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mpate kufanikiwa..} [AALI IIMRAN 200). Katika aya hii, Allah S.W. kwanza ameamrisha kusubiri na hakuishia hapo bali akaamrisha kushindana katika kusubiri.
MAREJEO:
Profesa. Mohamed Sayyed Ahmed Al-Mesayyar, Al Mujtamaa Al Mithaaliy fil Fikri Falsafiy wa Mawqif Islam minhu, Cairo: Dar AL-Maaref, Ch. 2, 1989, (Uk.139-142-188).