Ni ipi hukumu ya Uimamu wa mtoto kwa mtoto mwenzake katika Swala? Na je, inatofautiana ikiwa Swala ni ya faradhi au ya Sunna?
Soma zaidi....
Je, mwanamke anaweza kuwa Imamu wa wanaume katika Swala ya faradhi? Na je, inajuzu kwa mwanamke kuwaswalisha wanawake wenzake katika Swala ya faradhi? Na ni wapi atasimama kama Imamu iwapo ataswalisha wanawake?
Soma zaidi....
Je, nini hukumu ya kupeana mikono baada ya Swala baina ya waumini? Wapo baadhi ya watu wanaosema kuwa ni bid‘a kwa madai kwamba haikupokelewa kutoka kwa Mtume (S.A.W) wala Maswahaba zake watukufu, na kwamba inamshughulisha mswaliji na dhikiri za kumalizia Swala.
Soma zaidi....
Watu hunitanguliza mbele wakati Imamu rasmi anapokosekana ili niwaswalishe, kwa kuwa mimi nimehifadhi kiasi kikubwa cha Qur’ani Tukufu. Huenda nikasikia sauti ya mtu akiingia akitaka kupata rakaa kabla sijainuka kutoka kwenye rukuu, basi humsubiri kwa muda kidogo hadi aipate rakaa. Je, kitendo hiki ni halali kisharia?
Soma zaidi....
Nilipokuwa naswali siku moja Msikitini nilikuwa naachia mikono nikiwa nimesimama, baada ya kumaliza kuswali akanijia mtu mmoja na akaniambia: kwanini huweki mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto katika Swala? Nikamwambia: mimi naswali hivi tangu nilipoanza kuswali. akasema: kufanya hivi ni kinyume na Sunna. Ni upi usahihi wa maneno haya? Je, Swala yangu ni sahihi?
Soma zaidi....
Mtu yupo dukani anaswali peke yake, anauliza: je, analazimika kuweka kizuizi mbele yake akiwa anaswali?
Soma zaidi....
Baahi ya watu katika Msikiti wa mji wetu wanaweka nafasi zao maalumu kwa kuweka msala au mfano wake, hasa katika safu ya mbele, kwa namna nafasi hiyo inakuwa ya kwao muda wowote wanapofika msikitini, je, inafaa kwao kufanya hivyo?
Soma zaidi....
Nimeingia kuswali ya jamaa Msikitini Sawla ya Alasiri, nikakuta Imamu anasoma kwa sauti na hakusujudu sijida ya kusahau, je, hii ni Sahihi?
Soma zaidi....
Kuna baadhi ya watu wanaonipenda, je, kunajuzu kwangu kuwaombea dua katika Swala kwa kumtaja jina?
Soma zaidi....
Ni ipi hukumu ya Swala ya Ijumaa ikiafikiana na siku ya Idi? Je, Swala ya Ijumaa haitekelezwi ikiwa Idi ni siku ya Ijumaa? Na mnasemaje katika kutokutekeleza Swala ya Adhuhuri pia ikiwa Idi siku ya Ijumaa, kwa kutosheka na Swala ya Idi?
Soma zaidi....
“Je, hukumu ya Swala kwa mgonjwa wa Alzheimer (ugonjwa unaoathiri ubongo) ni ipi: je, huondolewa kwake? Na je, anatakiwa kuzilipa Swala alizoziacha pale anapopata fahamu tena?”
Soma zaidi....
“Mtu aliyeweza kushiriki katika Swala ya Ijumaa na akapata kusujudu mara mbili pamoja na tashahhud akiwa na Imamu, kisha Imamu alipotoa salamu akakamilisha mwenyewe rakaa mbili — je, kitendo chake hicho ni sahihi na je, kinamtosheleza kama Swala ya Ijumaa kisharia?
Soma zaidi....
Suala: Mtoto mwenye umri zaidi ya miaka kumi, anayeswali kwa ufasaha, huhudhuria msikitini, na hufika mapema kabla ya iqama kwa muda wa kutosha ili apate nafasi katika safu ya kwanza na kusimama humo. Je, mtoto huyu anapaswa kuondolewa katika nafasi yake aliyewahi na kusimama humo, ili watu wazima wengine wachukue nafasi hiyo?
Soma zaidi....
Niliingia msikitini kuswali Isha na nikawakuta watu wakiswali jamaa, nikaswali pamoja nao. Baada ya jamaa kumalizika, nikashangaa Imamu wa Swala akiniambia kuwa wao walikuwa wanaswali Sunna na si Swala ya Isha. Je, swala yangu ni sahihi?
Soma zaidi....
Mtu alisafiri kwenda nchini China kwa ajili ya kazi, na alipoenda msikitini kuswali alikuta muadhini anakimu Swala kwa kutumia lafudhi zilezile za Adhana, akirudia maneno na hakuyafanya mara moja, huku akiongeza «qad qāmatiṣ-ṣalāh», na anauliza: Hukumu ya iqama hii ni ipi? Na je, lafudhi hii imepokewa kutoka kwa Mtume (S.A.W)?
Soma zaidi....
Je, inajuzu kwa yeyote kati ya waumini kumtangulia Imamu rasmi wa Msikiti ikiwa yule anayetaka kutangulia ni mjuzi zaidi na ana elimu kubwa kuliko Imamu huyo?
Soma zaidi....
Nilikuwa safarini, na njiani gari lilisimama mahali pa kupumzika. Abiria walishuka ili kutekeleza ibada ya Swala, na nilikuwa nikihisi haja ya kwenda chooni, lakini niliiahirisha kutokana na msongamano katika vyoo. Hivyo, niliingia msikitini ili kuwahi Swala ya faradhi ya jamaa. Wakati wa Swala, sikuweza tena kujizuia, na unyenyekevu wangu katika Swala uliondoka kabisa. Hivyo, nilitoka kwenye Swala nikiwa nimeshikwa na dharura, nikaenda chooni. Je, ni ipi hukumu ya kutoka kwenye Swala kwa sababu hii?
Soma zaidi....
Ninataka kukamilisha (kuhitimisha) usomaji wa Qur'ani Tukufu katika Swala ya Tarawih ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, lakini sijahifadhi Qur'ani yote. Je, inaruhusiwa kwangu kusoma kwa kuangalia kwenye msahafu katika Swala?
Soma zaidi....
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
